Aayaat Za Qur-aan Kuhusu Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa

 

Aayaat Za Qur-aan Kuhusu Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa

 

Alhidaaya.com

 

Zifuatazo ni baadhi ya Aayaat ambazo Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى) Anasema kuhusu ‘Ilmu na fadhila zake mbalimbali:

 

 

 

1-‘Ilmu Humpandisha Mtu Daraja:

 

 

Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قِيلَ لَكُمْ تَفَسَّحُوا فِي الْمَجَالِسِ فَافْسَحُوا يَفْسَحِ اللَّـهُ لَكُمْ ۖ وَإِذَا قِيلَ انشُزُوا فَانشُزُوا يَرْفَعِ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ ۚ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ﴿١١﴾

Enyi walioamini! Mnapoambiwa: Fanyeni nafasi katika mabaraza, basi  fanyeni nafasi; Allaah Atakufanyieni nafasi. Na mnapoambiwa: Inukeni, basi inukeni; Allaah Atawainua wale walioamini miongoni mwenu na waliopewa elimu daraja za juu. Na Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Al-Mujaadalah: 11]

 

 

 

2-Wenye ‘Ilmu Wanashuhuduia Pamoja Na Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) Na Malaika Tawhiyd Ya Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾

Allaah Ameshuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye; na (pia) Malaika na wenye elimu (kwamba Allaah) ni Mwenye kusimamisha (uumbaji Wake) kwa uadilifu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Aal-‘Imraan: 18]

 

 

 

3-Hawalingani Sawa Mwenye ‘Ilmu Na Asiyekuwa Na ‘Ilmu

 

Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

أَمَّنْ هُوَ قَانِتٌ آنَاءَ اللَّيْلِ سَاجِدًا وَقَائِمًا يَحْذَرُ الْآخِرَةَ وَيَرْجُو رَحْمَةَ رَبِّهِ ۗ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٩﴾

Je, yule aliye mtiifu nyakati za usiku akisujudu, au akisimama (kuswali), anatahadhari na Aakhirah na anataraji rahmah ya Rabb wake (ni sawa na aliyekinyume chake?). Sema: Je, wanalingana sawa wale wanaouja na wale wasiojua? Hakika wanakumbuka wenye akili tu. [Az-Zumar: 9]

 

 

 

4-Aayaat Za Kwanza Na Amri Ya Kwanza Ilikuwa Ni Iqraa (Soma)!

 

Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ ﴿١﴾ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ ﴿٢﴾ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ ﴿٣﴾ الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ ﴿٤﴾ عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ ﴿٥﴾

Soma kwa Jina la Rabb wako Aliyeumba. Amemuumba mwana-Aadam kutokana na pande la damu linaloning’inia. Soma na Rabb wako ni Mkarimu kushinda wote. Ambaye Aliyefunza kwa kalamu. Amemfunza mwana-Aadam ambayo asiyoyajua. [Al-‘Alaq: 1-5]

 

 

 

 

5-Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) Ametanguliza Kutaja ‘Ilmu Kabla Ya Kuumba Mwana-Aadam:

 

Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

الرَّحْمَـٰنُ ﴿١﴾ عَلَّمَ الْقُرْآنَ ﴿٢﴾ خَلَقَ الْإِنسَانَ ﴿٣﴾ عَلَّمَهُ الْبَيَانَ ﴿٤﴾

Ar-Rahmaan. Amefundisha Qur-aan. Ameumba mwana-Aadam. Amemfunza ufasah

  

 

 

6-Wenye ‘Ilmu Ni Wenye Kumkhofu Allaah (عَزَّ وَجَلَّ)

 

Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

  إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ ۗ

Hakika wanaomkhofu Allaah miongoni mwa waja Wake ni ‘Ulamaa. [Faatwir: 28]

 

 

 

 

7-Amri Ya Kuomba Du’aa Ya Kuzidishiwa ‘Ilmu

 

Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

وَلَا تَعْجَلْ بِالْقُرْآنِ مِن قَبْلِ أَن يُقْضَىٰ إِلَيْكَ وَحْيُهُ ۖ وَقُل رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا ﴿١١٤﴾

wala usiiharakize Qur-aan (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kabla haikumalizwa kufunuliwa Wahy kwako. Na sema: Rabb wangu! Nizidishie elimu. [Twaahaa: 114]

 

 

 

8-Wenye ‘Ilmu Wanamkhofu Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) Huporomoka Kusujudu Kwa Kulia Na Kunyenyekea  

 

Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

قُلْ آمِنُوا بِهِ أَوْ لَا تُؤْمِنُوا ۚ إِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مِن قَبْلِهِ إِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ يَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ سُجَّدًا ﴿١٠٧﴾ وَيَقُولُونَ سُبْحَانَ رَبِّنَا إِن كَانَ وَعْدُ رَبِّنَا لَمَفْعُولًا ﴿١٠٨﴾ وَيَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ يَبْكُونَ وَيَزِيدُهُمْ خُشُوعًا ۩﴿١٠٩﴾

 

Sema: Iaminini au msiamini. Hakika wale waliopewa elimu kabla yake wanaposomewa (Qur-aan) wanaporomoka kifudifudi wanasujudu. Na wanasema: Utakasifu ni wa Rabb wetu; hakika ahadi ya Rabb wetu lazima itimizwe. Na wanaporomoka kifudifudi huku wanalia na inawazidishia unyenyekevu. [Al-Israa: 107 – 109]

 

 

9-Wenye ‘Ilmu Wanashuhuduia Yaliyoteremshwa Kuwa Ni Haki Na Yanaongoza Katika Njia Iliyonyooka:

 

Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

وَيَرَى الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ الَّذِي أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ هُوَ الْحَقَّ وَيَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ ﴿٦﴾

Na wale waliopewa elimu wanaona kuwa yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako ndio haki, na yanaongoza kwenye njia ya Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote.  [Sabaa: 6]

 

 

 

10-Wenye ‘Ilmu Hawana Shaka Na Hawatatizwi Na Aayat Mutashaabihaat

 

Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

 

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ ۖ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ ۗ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّـهُ ۗ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٧﴾

Yeye Ndiye Aliyeteremsha kwako Kitabu humo mna Aayaat zenye maana wazi, hizo ndio msingi wa Kitabu, na nyinginezo zisizokuwa wazi maana zake. Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotovu hufuata zile zisizokuwa wazi maana zake kutafuta fitnah (upotofu) na kutafuta maana zake zilofichika, na hakuna ajuae maana zake isipokuwa Allaah. Na wenye msingi madhubuti katika elimu husema: Tumeziamini, zote ni kutoka kwa Rabb wetu. Na hawakumbuki ila wenye akili [Aal-‘Imraan: 7]

 

 

Aayaat Muhkamaatun: Ni ambazo maana zake zinafahmika kiwepesi hazina mushkila wala utata na dalili zake ziko wazi. 

 

Aayaat Mutashaabihaat: Ni Aayah ambazo ni ngumu kufahamika, zinawatatanisha baadhi ya watu wasio na ‘ilmu ya kutosha.

 

 

Kisha baada ya kuamini, huomba Du’aa:

 

رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ ﴿٨﴾

(Husema): Rabb wetu, Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kuwa Umetuhidi na Tutunukie kutoka kwako rahmah. Hakika Wewe ni Mwingi wa kutunuku na kuneemesha. [Aal-‘Imraan: 9]

 

 

 

12-‘Ilmu Ni Uhai, Nuru, Ama Ujahili Ni Dhulma Na Shari.

 

Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

 أَوَمَن كَانَ مَيْتًا فَأَحْيَيْنَاهُ وَجَعَلْنَا لَهُ نُورًا يَمْشِي بِهِ فِي النَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُ فِي الظُّلُمَاتِ لَيْسَ بِخَارِجٍ مِّنْهَا ۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْكَافِرِينَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٢٢﴾

Je, aliyekuwa maiti kisha Tukamhuisha na Tukamjaalia nuru anatembea kwayo kati ya watu, ni sawa na yule ambaye yumo katika viza si mwenye kutoka humo? Hivyo ndivyo walivyopambiwa makafiri yale waliyokuwa wakiyatenda. [Al-An’aam: 122]

 

Hakika ‘Ilmu ni uhai na Nuru kwa sababu Nuru inamtoa mtu kizani na inabainisha ukweli wa mambo na kubakia kuwa wazi. Ama Ujahili ni dhulma dhidi ya Al-Khaaliq (Muumbaji) na hivyo inamfanya mtu abakie kizani asione haki wala asitambue sababu yake ya kuumbwa. (Rejea Suwrah Al-An’aam Aayah 1 – 3).

 

 

 

13-‘Ilmu Ni Hikmah Aliyejaaliwa Nayo Amejaaliwa Kheri Nyingi:

 

Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

يُؤْتِي الْحِكْمَةَ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُؤْتَ الْحِكْمَةَ فَقَدْ أُوتِيَ خَيْرًا كَثِيرًا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٢٦٩﴾

Humpa hikmah Amtakaye. Na anayepewa hikmah basi kwa yakini huwa amepewa khayr nyingi. Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili. [Al-Baqarah: 269]

 

 

 

14-‘Ilmu Ni Baswiyrah Ama Ujahili Ni Upofu

 

 

Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

 

قُلْ مَن رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ قُلِ اللَّـهُ ۚ قُلْ أَفَاتَّخَذْتُم مِّن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ لَا يَمْلِكُونَ لِأَنفُسِهِمْ نَفْعًا وَلَا ضَرًّا ۚ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ أَمْ هَلْ تَسْتَوِي الظُّلُمَاتُ وَالنُّورُ ۗ أَمْ جَعَلُوا لِلَّـهِ شُرَكَاءَ خَلَقُوا كَخَلْقِهِ فَتَشَابَهَ الْخَلْقُ عَلَيْهِمْ ۚ قُلِ اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ ﴿١٦﴾

Sema: Ni nani Rabb wa mbingu na ardhi? Sema: Ni Allaah. Sema: Je, mnawafanya wengineo badala Yake kuwa walinzi na hali hawamiliki kwa ajili ya nafsi zao manufaa wala dhara? Sema: Je, kipofu analingana sawa na mwenye kuona, au je, viza vinalingana sawa na nuru? Au wamemfanyia Allaah washirika walioumba kama uumbaji Wake, kisha yakafanana maumbile kwao?  Sema: Allaah ni Muumbaji wa kila kitu, Naye ni Mmoja Pekee, Asiyepingika. [Ar-Ra’d: 16]

 

 

Na Anasema pia Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

أَفَمَن يَعْلَمُ أَنَّمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ الْحَقُّ كَمَنْ هُوَ أَعْمَىٰ ۚ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿١٩﴾

Je, anayejua kwamba yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kutoka kwa Rabb wako ni haki ni sawa na ambaye yeye ni kipofu? Hakika wanazingatia wenye akili tu. [Ar-Ra’d: 19]

 

 

 

 

15-Umuhimu Wa Da’wah Kwa Wenye ‘Ilmu

 

Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

وَمَا كَانَ الْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا كَافَّةً ۚ فَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَائِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ﴿١٢٢﴾

Na haiwapasi Waumini watoke wote pamoja (kupigana jihaad). Basi kwanini lisitoke katika kila kundi miongoni mwao, kundi (moja tu) wajifunze vyema Dini na ili waonye watu wao watakaporejea kwao ili wapate kujihadharisha. [At-Tawbah: 122]

 

 

16-Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى) Amewasifia Na Kuthibitisha ‘Ulamaa Kuwa Wanahifadhi Aayaat Katika Vifua Vyao. Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

بَلْ هُوَ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ فِي صُدُورِ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ ۚ وَمَا يَجْحَدُ بِآيَاتِنَا إِلَّا الظَّالِمُونَ ﴿٤٩﴾

Bali hizo ni Aayaat bayana (zimehifadhika) katika vifua vya wale waliopewa elimu. Na hawazikanushi Aayaat Zetu isipokuwa madhalimu. [Al-‘Ankabuwt: 49]

 

 

 

 

Share