08-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Amri ya Kula Pambizoni Mwa Sahani na Kukatazwa Kula Katikati Yake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب الأمر بالأكل من جانب القصعة والنهي عن الأكل من وسطها

08-Mlango Wa Amri ya Kula Pambizoni Mwa Sahani na Kukatazwa Kula Katikati Yake

 

Alhidaaya.com

 

 

فِيهِ : قَوْله صلى الله عليه وسلم : ((  وَكُلْ مِمَّا يَلِيكَ )) متفق عَلَيْهِ كما سبق .

Ndani yake ni kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Na kula kilicho mbele yako." [Al-Bukhaariy na Muslim], kama ilivyotanguliwa kutajwa.

 

Hadiyth – 1

وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : ((  البَرَكَةُ تَنْزِلُ وَسَطَ الطعَامِ ؛ فَكُلُوا مِنْ حَافَتَيْهِ ، وَلاَ تَأكُلُوا مِنْ وَسَطِهِ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Baraka inashuka katikati ya chakula, kwa hivyo kuleni kwa pambizoni mwake na wala msile kutokea katikati yake." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na amesema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 2

وعن عبد الله بن بُسْرٍ رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ للنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَصْعَةٌ يُقَالُ لَهَا : الغَرَّاءُ يَحْمِلُهَا أرْبَعَةُ رجالٍ ؛ فَلَمَّا أضْحَوْا وَسَجَدُوا الضُّحَى أُتِيَ بِتِلْكَ الْقَصْعَةِ ؛ يعني وَقَدْ ثُردَ فِيهَا ، فَالتَفُّوا عَلَيْهَا ، فَلَمَّا كَثُرُوا جَثَا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم . فَقَالَ أعرابيٌّ : مَا هذِهِ الجِلْسَةُ ؟ فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((  إنَّ اللهَ جَعَلَنِي عَبْداً كَريماً ، وَلَمْ يَجْعَلْنِي جَبَّاراً عَنِيداً )) ، ثُمَّ قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : ((  كُلُوا مِنْ حَوَالَيْهَا ، وَدَعُوا ذِرْوَتَها يُبَارَكْ فِيهَا )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ جيد .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Busr (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na gudulia kubwa liliokuwa likiitwa Al-Gharraa'u na lilikuwa likibebwa na watu wanne. Baada ya Swahaaba kuswali Swalaah ya Dhuhaa, gudulia hili lilikuwa likiletwa likiwa limejaa Thariid (aina fulani ya mchuzi) na watakaa pambazoni mwake. Pindi wanapokuwa watu ni wengi, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikaa chini kwa magoti, mapaja yake na vidole vyake vya miguu vikigusa chini katika ardhi. Bedui akauliza: "Ni mkao gani huu mliokaa?" Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hakika Allaah amenijaalia mimi kuwa mja mtukufu (mwenye tabia nzuri) wala hakunijaalia kuwa mwenye kibri na kuchukua haki za watu pasi na haki yoyote." Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Kuleni pambazoni mwa gudulia na acheni sehemu iliyonyanyuka ya katikati na mtabarikiwa kwayo." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Jayd (nzuri)].

 

 

 

 

Share