09-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuchukiza Kula Kwa Kutegemea

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب كراهية الأكل متكئاً

09-Mlango Wa Kuchukiza Kula Kwa Kutegemea

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن أَبي جُحَيْفَةَ وَهْبِ بن عبد الله رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ آكُلُ مُتَّكِئاً )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Juhayfah Wahb bin 'Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mimi sili (chakula) nikiwa nimeegemea." [Al-Bukhaariy]

 

قَالَ الخَطَّابِيُّ : المُتَّكئُ هاهُنَا : هُوَ الجالِسُ مُعْتَمِداً عَلَى وِطَاءٍ تحته ، قَالَ : وأرادَ أنَّهُ لا يَقْعُدُ عَلَى الوِطَاءِ وَالوَسَائِدِ كَفِعْل مَنْ يُريدُ الإكْثَارَ مِنَ الطَّعَام ، بل يَقْعُدُ مُسْتَوفِزاً لاَ مُسْتَوطِئاً ، وَيَأكُلُ بُلْغَةً . هَذَا كلامُ الخَطَّابيِّ ، وأشارَ غَيْرُهُ إِلَى أنَّ الْمُتَّكِئَ هُوَ المائِلُ عَلَى جَنْبِه ، والله أعلم .

Amesema Al-Khatwaabiy: "Mwenye kutegemea hapa ni yule anayekaa kwa kuegemea mto ulio chini yake. Amesema: "Na kusudio ni kuwa yeye (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa ni mwenye kukaa juu ya mto kama kitendo cha mwenye kutaka kula zaidi (chakula kingi). Bali alikuwa akikaa wima sio mwenye kuegemea." Na ameashiria mwengine asiyekuwa yeye ya kwamba mwenye kuegemea ni yule anayejilaza kwa ubavu wake.

 

 

Hadiyth – 2

وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : رَأَيْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم جَالِساً مُقْعِياً يَأكُلُ تَمْراً . رواه مسلم .

Na amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Nimemuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameketi chini amenyanyua magoti yake akila tenda." [Muslim]

 

 

 

 

Share