02-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kujuzu Kulala kwa Maungo na Kuweka Mguu Mmoja juu ya Mwengine Ikiwa Hapana Hofu ya Kuonekana Utupu na Kujuzu Kukaa kwa Kukunja Mguu na Kufunga Kitambara Kiunini na Miguuni

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

 

باب جواز الاستلقاء عَلَى القفا ووضع إحدى الرِّجلين عَلَى الأخرى إِذَا لم يخف انكشاف العورة وجواز القعود متربعاً ومحتبياً

02-Mlango Wa Kujuzu Kulala kwa Maungo na Kuweka Mguu Mmoja juu ya Mwengine Ikiwa Hapana Hofu ya Kuonekana Utupu na Kujuzu Kukaa kwa Kukunja Mguu na Kufunga Kitambara Kiunini na Miguuni

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Hadiyth – 1

عن عبدِ اللهِ بن زيد رضي الله عنهما : أنَّه رأى رسولَ الله صلى الله عليه وسلم مُسْتَلْقِياً في الْمَسْجِدِ ، وَاضِعاً إحْدَى رِجْلَيْهِ عَلَى الأُخْرَى . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Zayd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba alimuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amelala kwa mgongo wake Msikitini na kuweka mguu wake mmoja juu ya mwengine." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن جابر بن سَمُرَة رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم إِذَا صَلَّى الفَجْرَ تَرَبَّعَ في مَجْلِسِهِ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ حَسْنَاء . حديث صحيح ، رواه أَبُو داود وغيره بأسانيد صحيحة .

Imepokewa kutoka kwa Jaabir bin Samurah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa baada ya kuswali Alfajiri akikaa kitako kwa kukunja miguu yake mpaka jua lichomoze kwa kuonekana mng'aro wake." [Hadiyth Swahiyh: Abu Daawuwd na wengineo kwa Isnaad Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 3

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : رأيتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم بفناءِ الكَعْبَةِ مُحْتَبِياً بِيَدَيْهِ هكَذا ، وَوَصَفَ بِيَدَيْهِ الاحْتِبَاءَ ، وَهُوَ القُرْفُصَاءُ . رواه البخاري .

Na amesema Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Nilimuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amekaa katika ukumbi wa Ka'bah na mikono yake imefunikwa hivi. Na akaonyesha kwa mikono yake jinsi alivyokaa kwa mikono yake kushika miguu iliyonyanyuliwa." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 4

وعن قَيْلَةَ بنْتِ مَخْرَمَةَ رضي الله عنها ، قالت : رأيتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ قَاعِدٌ القُرْفُصَاءَ ، فَلَمَّا رَأَيْتُ رسولَ الله المُتَخَشِّعَ في الجِلْسَةِ أُرْعِدْتُ مِنَ الفَرَقِ . رواه أَبُو داود والترمذي .

Na amesema Qaylah bint Makhramah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Nilimuona Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)akiwa amekaa na mikono yake ikishika miundi yake na mapaja juu amenyanyua. Na nilipomuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika hali ya kikao cha unyenyekevu nilitetemeka kwa hofu." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

 

 

Hadiyth – 5

وعن الشَّريدِ بن سُوَيْدٍ رضي الله عنه ، قَالَ : مَرَّ بي رسولُ الله صلى الله عليه وسلم وَأَنَا جَالِسٌ هكَذَا ، وَقَدْ وَضَعْتُ يَدِيَ اليُسْرَى خَلْفَ ظَهْرِي ، وَاتَّكَأتُ عَلَى أَليَةِ يَدي ، فَقَالَ : (( أَتَقْعُدُ قِعْدَةَ المَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ ؟! )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ صحيح .

Na amesema Shariyd bin Suwayd (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alinipita wakati mmoja Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nikiwa nimekaa hivi, nikiwa nimeuweka mkono wangu wa kushoto nyuma ya mgongo wangu na nikakaa chini juu ya matumbo ya vidole vyangu. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliponiona nimekaa hivi akasema: "Je, unakaa kama kikao cha walioghadhibikiwa (waliokasirikiwa)?" [Abu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]

 

 

Share