03-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Adabu za Kikao na Wenye Kukaa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب في آداب المجلس والجليس

03-Mlango Wa Adabu za Kikao na Wenye Kukaa

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لا يُقِيمَنَّ أحَدُكُمْ رَجُلاً مِنْ مَجْلِسِهِ ثُمَّ يَجْلِسُ فِيهِ ، وَلكِنْ تَوَسَّعُوا وَتَفَسَّحُوا )) وكَانَ ابْنُ عُمَرَ إِذَا قَامَ لَهُ رَجُلٌ مِنْ مَجْلِسِهِ لَمْ يَجْلِسْ فِيهِ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Asimpishe mmoja wenu mtu mwengine katika kikao chake kisha akakaa hapo, lakini toweni wasaa na toweni nafsi." Na alikuwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) anapompisha mtu katika kikazi chake, hakai tena hapo." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا قَامَ أَحَدُكُمْ مِنْ مَجْلِسٍ ، ثُمَّ رَجَعَ إِلَيْهِ ، فَهُوَ أَحَقُّ بِهِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Akisimama mmoja wenu kutoka katika kikao chake kisha akakirudia huyo ana haki zaidi ya kikao hicho (kuliko mwengine yeyote)." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن جابر بن سَمُرَة رضي الله عنهما ، قَالَ : كُنَّا إِذَا أَتَيْنَا النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، جلَسَ أحَدُنَا حَيْثُ يَنْتَهِي . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Na amesema Jaabir bin Samurah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Tulikuwa tunapomwendea Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hukaa mmoja wetu mahali ambapo litamuweka kwake baraza." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي عبد الله سَلْمَان الفارسي رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم :(( لاَ يَغْتَسِلُ رَجُلٌ يَوْمَ الْجُمُعَةِ، وَيَتَطهَّرُ مَا اسْتَطَاعَ مِنْ طُهْرٍ ، وَيَدَّهِنُ مِنْ دُهْنِهِ، أَوْ يَمَسُّ مِنْ طِيب بَيْتِهِ ، ثُمَّ يَخْرُجُ فَلاَ يُفَرِّقُ بَيْنَ اثْنَينِ ، ثُمَّ يُصَلِّي مَا كُتِبَ لَهُ ، ثُمَّ يُنْصِتُ إِذَا تَكَلَّمَ الإمَامُ ، إِلاَّ غُفِرَ لَهُ مَا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الجُمُعَةِ الأُخْرَى )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu 'Abdillaah Salmaan Al-Faarisiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Haogi mmoja wenu siku ya Ijumaa na akajitwahirisha kadri ya uwezo wake na akajitia nyumbani kwake manukato kisha akaenda Msikitini na akawa hapasuwi safu kati ya watu wawili, kisha akaswali kiasi chake, kisha akakaa kimya akamsikia Imamu wakati akizungumza (akitoa Khutbah) isipokuwa atasamehewa kuanzia Ijumaa ile mpaka nyingine." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 5

وعن عمرو بن شُعَيْب، عن أبيهِ، عن جَدِّهِ رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لاَ يَحِلُّ لِرَجُلٍ أنْ يُفَرِّقَ بَيْنَ اثْنَيْنِ إِلاَّ بإذْنِهِمَا )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال: (( حديث حسن )) 

وفي رواية لأبي داود : (( لاَ يُجْلسُ بَيْنَ رَجُلَيْنِ إِلاَّ بِإذْنِهِمَا ))

Imepokewa kutoka kwa 'Amru bin Shu'ayb kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Si halali kwa mtu yeyote kuwatenganisha kati ya watu wawili ila kwa idhini yao." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

Na katika riwaayah ya Abu Daawuwd: "Hakika mtu baina ya watu wawili ila kwa idhini yao." 

 

 

Hadiyth – 6

وعن حذيفة بن اليمان رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم لَعَنَ مَنْ جَلَسَ وَسَطَ الحَلْقَةِ . رواه أَبُو داود بإسنادٍ حسن .

وروى الترمذي عن أبي مِجْلَزٍ : أنَّ رَجُلاً قَعَدَ وَسَطَ حَلْقَةٍ ، فَقَالَ حُذَيْفَةُ : مَلْعُونٌ عَلَى لِسَانِ مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم - أَوْ لَعَنَ اللهُ عَلَى لِسَانِ مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم - مَنْ جَلَسَ وَسَطَ الحَلْقَةِ . قَالَ الترمذي : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Hudhayfah bin Al-Yamaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimlaani mtu mwenye kukaa katikati ya duara ya watu." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy kwa Isnaad Hasan]

Amepokea At-Tirmidhiy kutoka kwa Abu Mijlaz kwamba kulikuwa na mtu aliyekaa katikati ya duara, Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhu) akasema: "Amelaaniwa katika ulimi wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) au Allaah amemlaani kutoka kwa ulimi wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), mwenye kukaa katikati ya duara." [Amesema At-Tirmidhiy kuwa hii ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي سعيدٍ الخدريِّ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( خَيْرُ المَجَالِسِ أوْسَعُهَا )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ صحيح عَلَى شرط البخاري .

Na amesema Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Bora ya vikao ni vyenye wasaa." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh kulingana na sharti ya Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 8

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ جَلَسَ في مَجْلِسٍ ، فَكَثُرَ فِيهِ لَغَطُهُ فَقَالَ قَبْلَ أنْ يَقُومَ مِنْ مَجْلِسِهِ ذَلِكَ : سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ ، أشْهَدُ أنْ لا إلهَ إِلاَّ أنْتَ ، أسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوبُ إلَيْكَ ، إِلاَّ غُفِرَ لَهُ مَا كَانَ في مَجْلِسِهِ ذَلِكَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote anayekaa katika baraza na mazungumzo yakawa mengi (yasiyo mfaidisha Aakhera yake), akawa ni mwenye kusema kabla ya kuondoka kwenye kikazi hicho: 'Subhaanaka Allaahumma wa Bihamdika Ashhadu an Laa Illaaha illa Anta Astaghfiruka wa Atuubu Ilayka - Kutakasika na maovu ni Kwako Ee Rabb wangu wa haki pamoja na sifa Zako nzuri nakiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kwamba hapana Rabb mwenye haki ya kuabudiwa ila Wewe nakuomba msamaha na ninarudi Kwako,' isipokuwa husamehewa yale yaliokuwa katika kikao hicho." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 9

وعن أَبي بَرْزَة رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم يقولُ بأَخَرَةٍ إِذَا أرَادَ أنْ يَقُومَ مِنَ الْمَجْلِسِ : (( سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وبِحَمْدِكَ ، أشْهَدُ أنْ لا إلهَ إِلاَّ أنتَ أسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوبُ إليكَ )) فَقَالَ رَجُلٌ : يَا رسولَ الله ، إنَّكَ لَتَقُولُ قَوْلاً مَا كُنْتَ تَقُولُهُ فِيمَا مَضَى ؟ قَالَ : (( ذَلِكَ كَفَّارَةٌ لِمَا يَكُونُ في المَجْلِسِ )) رواه أَبُو داود ، ورواه الحاكم أَبُو عبد الله في " المستدرك " من رواية عائشة رضي الله عنها وقال : (( صحيح الإسناد )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Barzah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema mwisho wa umri wake dua ifuatayo pindi alipokuwa anasimama kuondoka katika baraza: "Subhaanaka Allaahumma wa Bihamdika Ashhadu an Laa Illaah illa Anta Astaghfiruka wa Atuubu Ilayka." "Kutakasika na maovu ni Kwako Ee Rabb wangu wa haki pamoja na sifa Zako nzuri nakiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kwamba hapana Rabb mwenye haki ya kuabudiwa ila Wewe nakuomba msamaha na ninarudi Kwako." Akasema mtu mmoja: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika wewe unasema maneno ambayo hukuwa ukiyasema kabla." Akasema: "Hiyo ni kafara kwa yanayotendeka katika baraza." [Abu Daawuwd na Al-Haakim Abu 'Abdillaah katika Al-Mustadrak yake kwa riwaayah ya 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) na akasema kuwa Isnaad yake ni Swahiyh].

 

 

Hadiyth – 10

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : قَلَّمَا كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم يَقُومُ مِنْ مَجْلِسٍ حَتَّى يَدْعُوَ بِهؤلاء الدَّعَواتِ : (( اللَّهُمَّ اقْسِمْ لَنَا مِنْ خَشْيَتِكَ مَا تَحُولُ بِهِ بَيْنَنَا وَبَيْنَ مَعَاصِيكَ ، وَمِنْ طَاعَتِكَ مَا تُبَلِّغُنَا بِهِ جَنَّتَكَ ، وَمِنَ الْيَقِينِ مَا تُهَوِّنُ عَلَيْنَا مَصَائِبَ الدُّنْيَا ، اللَّهُمَّ مَتِّعْنَا بأسْمَاعِنا ، وَأَبْصَارِنَا ، وقُوَّتِنَا مَا أحْيَيْتَنَا ، وَاجْعَلْهُ الوارثَ مِنَّا ، وَاجْعَلْ ثَأرَنَا عَلَى مَنْ ظَلَمَنَا ، وَانْصُرْنَا عَلَى مَنْ عَادَانَا ، وَلاَ تَجْعَلْ مُصيبَتَنَا فِي دِينِنَا ، وَلاَ تَجْعَلِ الدُّنْيَا أَكْبَرَ هَمِّنَا ، وَلاَ مَبْلَغَ عِلْمِنَا ، وَلاَ تُسَلِّطْ عَلَيْنَا مَنْ لاَ يَرْحَمُنَا )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba: Ilikuwa nadra sana kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuondoka katika kikao bila kuomba dua ifwatayo: "Allaahummaqsim Lanaa min Khashyatika maa tahuulu bihi baynana wa bayna Ma'aswiyka. Wa min Twaa'atika maa Tubalighunaa bihi Janattaka wa minal yaqiyni maa Tuhawwinu 'alayna maswaa'ibud Dunya. Allaahumma matti'naa biasmaa'inaa wa Abswaarinaa wa quwwatinaa maa ahyaytanaa waj'alhul waaritha minna waj'al tha'ranaa 'alaa man dhalamana wansurnaa 'alaa man 'aadaanaa walaa taj'al muswiibatanaa fii Diyninaa walaa taj'alid Dunya akbara hamminaa walaa mablagha 'ilminaa walaa tusallitw 'alayna man laa yarhamunaa." "Ee Rabb wangu! Tupatie hofu kubwa Kwako ambayo itakuwa ni kikwazo baina yetu na maasia; na kukutii Wewe ambako kutatusaidia kupata Pepo Yako; na Utupatie yakini (na Imaani) ambayo itatusaidia katika masikizi yenu na kuona kwetu na nguvu zetu maadamu Umetupatia uhai na Utujaalie ni warithi (na tufaidike) kwazo; na Ujaalie uchungu kutoka kwetu kwa wenye kutudhulumu, na Utusaidie dhidi ya maadui zetu; wala Usitujaalie kuwa na misiba katika Dini yetu; na Usitufanye dunia kuwa hamu yetu kubwa wala Usiiwinje elimu yetu na Usituchagulie kiongozi juu yetu ambaye hataturehemu." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

   

 

 

Hadiyth – 11

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا مِنْ قَوْمٍ يَقُومُونَ مِنْ مَجْلِسٍ لاَ يَذْكُرُونَ الله تَعَالَى فِيهِ ، إِلاَّ قَامُوا عَنْ مِثْل جِيفَةِ حِمَارٍ ، وَكَانَ لَهُمْ حَسْرَةٌ )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ صحيح .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna kaumu yeyote itainuka katika kikazi (kikao) ambacho hakimtaji Allaah Ta'aalaa ndani yake isipokuwa wanainuka (kuondoka) mfano wa punda mfu na watakuwa na majuto makuu kwao." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 12

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَا جَلَسَ قَوْمٌ مَجْلِساً لَمْ يَذْكُرُوا الله تَعَالَى فِيهِ ، وَلَمْ يُصَلُّوا عَلَى نَبِيِّهِمْ فِيهِ ، إِلاَّ كَانَ عَلَيْهِمْ تِرَةٌ ؛ فَإنْ شَاءَ عَذَّبَهُمْ ، وَإنْ شَاءَ غَفَرَ لَهُمْ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kaumu haitakaa katika kikao ambacho ndani yake hatajwi Allaah Ta'aalaa wala hawamswalii Nabiy wao isipokuwa watakumbwa na upungufu. Akipenda Atawaadhibu na akipenda Atawasamehe." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 13

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ قَعَدَ مَقْعَداً لَمْ يَذْكُر الله تَعَالَى فِيهِ كَانَتْ عَلَيْهِ مِنَ اللهِ تِرَةٌ ، وَمَنْ اضْطَجَعَ مَضْجَعَاً لاَ يَذْكُرُ الله تَعَالَى فِيهِ كَانَتْ عَلَيْهِ مِنَ اللهِ تِرَةٌ )) رواه أَبُو داود .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anayekaa kikao chochote kile asimdhukuru Allaah katika kikao hicho basi ana dhambi kutoka kwa Allaah, na anayelala sehemu yeyote ile kisha asimdhukuru Allaah wakati wakuinuka sehemu hiyo basi ana dhambi kwa Allaah." [Abu Daawuwd]

 

 

 

 

Share