12-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kumuombea Dua Aliyekwenda Chafya Anapomuhimidi Allaah Ta'aalaa na Karaha ya Kumuombea Ikiwa Hakumuhimidi Allaah Ta'aalaa na Kubainisha Adabu Unapopiga Chafya na Kupiga Miayo

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب استحباب تشميت العاطس إِذَا حمد الله تَعَالَى وكراهة تشميته إذا لَمْ يحمد الله تَعَالَى

وبيان آداب التشميت والعطاس والتثاؤب

12-Mlango Wa Kupendeza Kumuombea Dua Aliyekwenda Chafya Anapomuhimidi Allaah Ta'aalaa na Karaha ya Kumuombea Ikiwa Hakumuhimidi Allaah Ta'aalaa na Kubainisha Adabu Unapopiga Chafya na Kupiga Miayo

 

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّ الله يُحِبُّ العُطَاسَ ، وَيَكْرَهُ التَّثَاؤُبَ ، فَإذَا عَطَسَ أَحَدُكُمْ وَحَمِدَ الله تَعَالَى كَانَ حَقّاً عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ سَمِعَهُ أنْ يَقُولَ لَهُ : يَرْحَمُكَ اللهُ ، وَأَمَّا التَّثَاؤُبُ فَإنَّمَا هُوَ مِنَ الشَّيْطَانِ ، فَإذَا تَثَاءبَ أحَدُكُمْ فَلْيَرُدَّهُ مَا اسْتَطَاعَ ، فَإنَّ أحَدَكُمْ إِذَا تَثَاءبَ ضَحِكَ مِنْهُ الشَّيْطَانُ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah anapenda chafya na anachukia miayo. Hivyo, anapochemua mmoja wenu na akamshukuru Allaah Ta'aalaa inakuwa ni haki kwa Muislamu mwenye kusikia kumwambia: "Yarhamuka Allaah (Allaah Akurehemu)." Ama kuhusu kwenda miayo, hakika inatokana na shetani. Hivyo, anapokwenda miayo mmoja wenu ajaribu kujizui, kwani anayekwenda miyao huchekwa na shetani." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا عَطَسَ أحَدُكُمْ فَلْيَقُلْ : الحَمْدُ للهِ ، وَلْيَقُلْ لَهُ أخُوهُ أَوْ صَاحِبُهُ : يَرْحَمُكَ الله . فإذَا قَالَ لَهُ : يَرْحَمُكَ اللهُ ، فَليَقُلْ : يَهْدِيكُمُ اللهُ وَيُصْلِحُ بَالَكُمْ )) رواه البخاري .

Na Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapopiga chafya mmoja wenu aseme: "Alhamdulillaah (Kuhimidiwa ni kwa ni kwa Allaah)." Na aseme nduguye au sahibu yake: 'Yarhamka Allaah', naye aseme: 'Yahdikumu Allaahu wa Yuslih Baalakum (Allaah akuongozeni na akutengezeeni hali yenu)'." [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي موسى رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقولُ : (( إِذَا عَطَسَ أحَدُكُمْ فَحَمِدَ اللهَ فَشَمِّتُوهُ، فَإنْ لَمْ يَحْمَدِ الله فَلاَ تُشَمِّتُوهُ )) رواه مسلم.

Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-'Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Anapokwenda chafya mmoja wenu na akamshukuru Allaah (kwa kusema Alhamdulillaah)  asi muombeeni dua na ikiwa hakumshukuru Allaah basi hamuna haja ya kumuombea." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 4

وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : عَطَسَ رَجُلانِ عِنْدَ النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَشَمَّتَ أَحَدَهُمَا وَلَمْ يُشَمِّتِ الآخَرَ ، فَقَالَ الَّذِي لَمْ يُشَمِّتْهُ : عَطَسَ فُلانٌ فَشَمَّتَّهُ ، وَعَطَسْتُ فَلَمْ تُشَمِّتْنِي ؟ فَقَالَ : (( هَذَا حَمِدَ الله ، وَإنَّكَ لَمْ تَحْمَدِ الله )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Walikwenda chafya watu wawili mbele ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akamuombea dua mmoja wao na hakumuombea yule mwengine. Akasema yule ambaye hakuombewa dua: "Amekwenda chafya fulani nawe ukamuombea dua na mimi nimepiga chafya na hukuniombea." Akasema: "Huyu amemshukuru Allaah amesema: (Alhamdulillaah) na wewe hukumshukuru Allaah." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy] 

 

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم إِذَا عَطَسَ وَضَعَ يَدَهُ أَوْ ثَوْبَهُ عَلَى فِيهِ ، وَخَفَضَ - أَوْ غَضَّ - بِهَا صَوْتَهُ . شك الراوي . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anapokwenda chafya akiweka mkono wake ili kuhafifisha sauti yake (au kuuma). Ametia shaka mpokezi. [Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh].

 

 

Hadiyth – 6

وعن أَبي موسى رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ اليَهُودُ يَتَعَاطَسُونَ عِنْدَ رسول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يَرْجُونَ أنْ يَقُولَ لَهُمْ : يَرْحَمُكُم الله ، فَيَقُولُ : (( يَهْدِيكُم اللهُ وَيُصْلِحُ بَالَكُمْ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Walikuwa Mayahudi wakienda chafya mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakitarajia ya kwamba atawaambia: "Yarhamuka Allaah." Lakini alikuwa akisema: "Yahdiikumu Allaahu wa Yuslih Baalakum." [Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا تَثَاءبَ أحَدُكُمْ فَلْيُمْسِكْ بِيَدِهِ عَلَى فِيهِ ؛ فَإنَّ الشَّيْطَانَ يَدْخُلُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapokwenda  miayo mmoja wenu aufinike mdomo wake kwa mkono wake, kwani usipofanya hivyo shetani ataingia." [Muslim]

 

 

 

Share