11-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kubainisha Kuwa Sunnah kwa Mwenye Kubisha Anapoulizwa: "Nani?" Asema: "Fulani", Alitaje Jina Lake Linalijulikana au Kun-yah (Jina la Utani) na Karaha ya Kusema: "Mimi" na Mfano Wake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

 

باب بيان أنَّ السنة إِذَا قيل للمستأذن : من أنت ؟

أن يقول : فلان ، فيسمي نفسه بما يعرف به من اسم أَوْ كنية

وكراهة قوله : (( أنا )) ونحوها

11-Mlango Wa Kubainisha Kuwa Sunnah kwa Mwenye Kubisha Anapoulizwa: "Nani?" Asema: "Fulani", Alitaje Jina Lake Linalijulikana au Kun-yah (Jina la Utani) na Karaha ya Kusema: "Mimi" na Mfano Wake

 

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

وعن أنس رضي الله عنه في حديثه المشهور في الإسراءِ ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( ثُمَّ صَعَدَ بي جِبْريلُ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا فَاسْتَفْتَحَ ، فقِيلَ : مَنْ هذَا ؟ قَالَ : جِبْريلُ، قِيلَ : وَمَنْ مَعَكَ ؟ قَالَ : مُحَمَّدٌ ، ثُمَّ صَعَدَ إِلَى السَّمَاءِ الثَّانِيَةِ فاسْتَفْتَحَ ، قِيلَ : مَنْ هَذَا ؟ قَالَ : جِبْريل ، قِيلَ : وَمَنْ مَعَكَ ؟ قَالَ : مُحَمَّدٌ وَالثَّالِثَةِ وَالرَّابِعَةِ وَسَائِرِهنَّ وَيُقَالُ فِي بَابِ كُلِّ سَمَاءٍ : مَنْ هَذَا ؟ فَيَقُولُ : جِبْريلُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Anas katika Hadiyth mashuhuri ya Israa' amesema: kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kisha akapanda nami Jibriyl mpaka wingu wa dunia (wingu wa kwanza), akataka mlango ufunguliwa." Akaulizwa: "Nani huyo?" Akasema: "Jibriyl". Pakasemwa: "Na uko pamoja na nani?" Akasema: "Muhammad". Kisha akapanda nami Jibriyl wingu wa pili, na wa tatu, na wa nne na nyingine zote. Na alikuwa akiulizwa katika kila mlango wa wingu: "Ni nani huyu?" Naye akijibu: "Jibriyl". [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي ذرٍّ  رضي الله عنه ، قَالَ : خَرَجْتُ لَيْلَةً مِنَ اللَّيَالِي ، فَإذَا رسول الله صلى الله عليه وسلم يَمْشِي وَحْدَهُ، فَجَعَلْتُ أمْشِي فِي ظلِّ القمَرِ، فَالْتَفَتَ فَرَآنِي ، فَقَالَ: (( مَنْ هَذَا ؟ )) فقلتُ : أَبُو ذَرٍّ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Nilitoka usiku mmoja na kumuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akitembea peke yake. Nikawa mimi natembea katika kivuli cha mwezi. Alizunguka Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kuniona, akasema: "Ni nani huyu?" Nikasema: "Abu Dharr." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن أُمِّ هانىءٍ رضي الله عنها ، قالت : أتيتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يَغْتَسِلُ وَفَاطِمَةُ تَسْتُرُهُ ، فَقَالَ : (( مَنْ هذِهِ ؟ )) فقلتُ : أنا أُمُّ هَانِىءٍ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ummu Haani' (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba amesema: Nilikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa naoga na Faatwimah anamsitiri (kwa pazia). Akasema: "Nani huyu?" Nikasema: "Ni mimi Ummu Haani'." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 4

وعن جابر رضي الله عنه ، قَالَ : أتَيْتُ النبيَّ صلى الله عليه وسلم فَدَقَقْتُ البَابَ ، فَقَالَ : (( مَنْ هَذَا ؟ )) فَقُلتُ : أَنَا ، فَقَالَ : (( أنَا ، أنَا ! )) كَأنَّهُ كَرِهَهَا . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilimwendea Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nikagonga mlango akauliza: "Nani huyo?" Nikamjibu: "Mimi". Akasema: "Mimi, mimi!" kama vile amelichukia jibu hilo. [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

 

 

 

 

Share