32-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kusujudu Sijda ya Kushukuru (Sijdatus-Shukr) Unapopata Neema ya Wazi au Kuondokewa na Balaa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

 

باب استحباب سجود الشكر

عِنْدَ حصول نعمة ظاهرة أَو اندفاع بلية ظاهرة

32-Mlango Wa Kupendeza Kusujudu Sijda ya Kushukuru (Sijdatus-Shukr) Unapopata Neema ya Wazi au Kuondokewa na Balaa

 

Alhidaaya.com

 

 

عن سعد بن أَبي وقاص رضي اللهُ عنه ، قَالَ : خَرَجْنَا مَعَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم مِنْ مَكّةَ نُريدُ المَدِينَةَ ، فَلَمَّا كُنَّا قَرِيباً مِنْ عَزْوَرَاءَ نَزَلَ ثُمَّ رَفَعَ يَدَيْهِ فَدَعَا الله سَاعَةً ، ثُمَّ خَرَّ سَاجِداً ، فَمَكَثَ طَويلاً ، ثُمَّ قَامَ فَرَفَعَ يَدَيْهِ سَاعَةً ، ثُمَّ خَرَّ سَاجِداً - فَعَلَهُ ثَلاثَاً - وقال : (( إنِّي سَألتُ رَبِّي ، وَشَفَعْتُ لأُمَّتِي ، فَأعْطَانِي ثُلُثَ أُمَّتِي ، فَخَرَرْتُ سَاجِداً لِرَبِّي شُكْراً ، ثُمَّ رَفَعْتُ رَأسِي ، فَسَألْتُ رَبِّي لأُمَّتِي ، فَأعْطَانِي ثُلُثَ أُمَّتِي، فَخَرَرْتُ سَاجِداً لِرَبِّي شُكْراً ، ثُمَّ رَفَعْتُ رَأسِي ، فَسَألْتُ رَبِّي لأُمَّتِي ، فَأعْطَانِي الثُّلثَ الآخَرَ ، فَخَرَرْتُ سَاجِداً لِرَبِّي )) رواه أَبُو داود .

Amesema Sa'ad bin Abu Waqqaas (Radhwiya Allaahu 'anhu) : Tulitoka pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Makkah kwenda Madiynah. Tulipokuwa karibu na 'Azwaraa', alishuka, kisha akainua mikono yake, akamuomba Allaah kwa muda, kisha akasujudu muda mrefu kisha akasimama akainua mikono yake kwa muda, kisha akasujudu - akaifanya mara tatu-akasema: "Hakika nimeomba Rabb wangu, na nimeombea shafaa Ummah wangu. Amenipa thuluthi ya Ummah wangu, Nikasujudu kumshukuru Rabb wangu, kisha nikainua kichwa changu, nikamuomba Rabb wangu kwa ajili ya Ummah wangu. Akanipa thuluthi ya Ummah wangu, nikasujudu kumshukuru Rabb wangu, Kisha nikainua kichwa changu, nikamuomba Rabb wangu kwa ajili ya Ummah wangu, Akanipa thuluthi ya mwisho, Nikamsujudia Rabb wangu."  [Abuu Daawuwd]

 

Share