31-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ubora wa Siku ya Ijumaa na Wajibu wa Kuoga Kwayo na Kujipaka Manukato,Kwenda Mapema,Kuomba Dua Siku ya Ijumaa, Kumswalia Nabiy na Kubainisha Wakati wa Kujibiwa Dua,Kupendeza Kukithirisha Kumtaja Allaah Baada ya Ijumaa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فضل يوم الجمعة ووجوبها والاغتسال لَهَا

والطّيب والتبكير إِلَيْهَا والدعاء يوم الجمعة والصلاة

عَلَى النبي صلى الله عليه وسلم وفِيهِ بيان ساعة الإجابة

واستحباب إكثار ذكر الله تعالى بعد الجمعة

31-Mlango Wa Ubora wa Siku ya Ijumaa na Wajibu wa Kuoga Kwayo na Kujipaka Manukato, Kwenda Mapema, Kuomba Dua Siku ya Ijumaa, Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Kubainisha Wakati wa Kujibiwa Dua, Kupendeza Kukithirisha Kumtaja Allaah Baada ya Ijumaa

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ اللَّـهِ وَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ﴿١٠﴾

Na inapomalizika Swalaah, basi tawanyikeni katika ardhi, na tafuteni Fadhila za Allaah, na mdhukuruni Allaah kwa wingi ili mpate kufaulu. [Al-Jumua'ah: 10]

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( خَيْرُ يَومٍ طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ يَوْمُ الجُمُعَةِ : فِيهِ خُلِقَ آدَمُ ، وَفِيهِ أُدْخِلَ الجَنَّةَ ، وَفِيهِ أُخْرِجَ مِنْهَا )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Siku bora ya zilizochomozewa na jua ni siku ya Ijumaa, ndani yake aliumbwa Aadam na ndani yake aliingizwa Peponi na ndani yake alitolewa humo." [Muslim].

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ تَوَضَّأ فَأَحْسَنَ الوُضُوءَ ثُمَّ أتَى الجُمُعَةَ ، فَاسْتَمَعَ وأنْصَتَ ، غُفِرَ لَهُ مَا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الجُمُعَةِ وَزِيادَةُ ثَلاَثَةِ أيَّامٍ ، وَمَنْ مَسَّ الحَصَى ، فَقَدْ لَغَا )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yeyote atakayetawadha vizuri, kisha akaja Msikitini kwa ajili ya Swalaah ya Ijumaa. Akasikiliza na akanyamaza (katika kufanya hivyo), atasamehewa madhambi yake kuanzia Ijumaa iliyopita na Ijumaa hii na ziada ya siku tatu. Na yeyote atakayegusa vijiwe na kucheza navyo amefanya upuuzi." [Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( الصَّلَوَاتُ الخَمْسُ ، وَالجُمُعَةُ إِلَى الجُمُعَةِ ، وَرَمَضَانُ إِلَى رَمَضَانَ ، مُكَفِّراتٌ مَا بَيْنَهُنَّ إِذَا اجْتُنِبَتِ الكَبَائِرُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Swalaah tano (za faradhi) na Ijumaa mpaka Ijumaa na Ramadhwaan mpaka Ramadhwaan inafuta madhambi yaliyo madogo baina yake ikiwa dhambi kubwa zitaepukwa." [Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة ، وعن ابن عمر رضي الله عنهم : أنهما سَمعَا رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقولُ عَلَى أعْوَادِ مِنْبَرِهِ : (( لَيَنْتَهِيَنَّ أقْوَامٌ عَنْ وَدْعِهِمُ الجُمُعَاتِ أَوْ لَيَخْتِمَنَّ اللهُ عَلَى قُلُوبِهِمْ ثُمَّ لَيَكُونَنَّ مِنَ الغَافِلِينَ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah na Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhum) kuwa walimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema akiwa juu ya mimbar yake ya mbao: "Watu watakoma kuacha kwao Ijumaa, au Allaah atapiga muhuri mioyo yao, kisha watakuwa miongoni mwa walioghafilika." [Muslim]

 

Hadiyth – 5

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا جَاءَ أَحَدُكُمُ الجُمُعَةَ فَلْيَغْتَسِلْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mmoja wenu anapokwenda kwenye Swalaah ya Ijumaa na akoge." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 6

وعن أَبي سعيد الخدري رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( غُسْلُ يَوْمِ الجُمُعَةِ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُحْتَلِمٍ )) متفقٌ عَلَيْهِ 

Abuu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allahu 'anhu) amesema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kuoga siku ya Ijumaa ni wajibu kwa kila baleghe." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na An-Nasaai]

 

Hadiyth – 7

وعن سَمُرَةَ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ تَوَضَّأَ يَوْمَ الجُمُعَةِ فبِها وَنِعْمَتْ وَمَن اغْتَسَلَ فَالغُسْلُ أفْضَلُ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن ))

Imepokewa kutoka kwa Samurah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kutawadha siku ya Ijumaa, hiyo ni neema (nzuri), na mwenye kuoga ni bora zaidi." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 8

وعن سَلمَان رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( لاَ يَغْتَسِلُ رَجُلٌ يَومَ الجُمُعَةِ ، وَيَتَطَهَّرُ مَا اسْتَطَاعَ مِن طُهْرٍ ، وَيَدَّهِنُ مِنْ دُهْنِهِ ، أَوْ يَمَسُّ مِنْ طِيبِ بَيْتِهِ ، ثُمَّ يَخْرُجُ فَلاَ يُفَرِّقُ بَيْنَ اثنَيْنِ ، ثُمَّ يُصَلِّي مَا كُتِبَ لَهُ ، ثُمَّ يُنْصِتُ إِذَا تَكَلَّمَ الإمَامُ ، إِلاَّ غُفِرَ لَهُ مَا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الجُمُعَةِ الأُخْرَى )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Salmaan Al-Faarisiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Haogi mmoja wenu siku ya Ijumaa na akajitwahirisha kadiri ya uwezo wake na akajitia manukato nyumbani kwake kisha akaenda Msikitini na akawa hapasuwi safu kati ya watu wawili, kisha akaswali kiasi chake, kisha akakaa kimya akimsikiliza Imamu wakati akizungumza (akitoa Khutbah) isipokuwa atasamehewa kuanzia Ijumaa ile mpaka nyingine." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 9

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَن اغْتَسَلَ يَومَ الجُمُعَةِ غُسْلَ الجَنَابَةِ ، ثُمَّ رَاحَ في الساعة الأولى فَكَأنَّمَا قَرَّبَ بَدَنَةً ، وَمَنْ رَاحَ في السَّاعَةِ الثَّانِيَةِ ، فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَقَرَةً ، وَمَنْ رَاحَ في الساعة الثَّالِثَةِ ، فَكَأنَّمَا قَرَّبَ كَبْشاً أقْرَنَ ، وَمَنْ رَاحَ في السَّاعَةِ الرَّابِعَةِ ، فَكَأنَّمَا قَرَّبَ دَجَاجَةً ، وَمَنْ رَاحَ في السَّاعَةِ الخَامِسَةِ ، فَكَأنَّمَا قَرَّبَ بَيْضَةً ، فَإذَا خَرَجَ الإمَامُ ، حَضَرَتِ المَلاَئِكَةُ يَسْتَمِعُونَ الذِّكْرَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuoga siku ya Ijumaa kama anavyooga janaba kisha akaondoka (kuelekea kwenye Swalaah ya Ijumaa katika saa za mwanzo) basi atakuwa ni kama ametoa ngamia swadaqah. Na atakayekwenda katika saa ya pili basi atakuwa ni kama aliyetoa ng'ombe swadaqah, na atakayeondoka wakati wa saa ya tatu kama ametoa kondoo mwenye pembe swadaqah, na mwenye kuondoka wakati wa saa ya nne kama ametoa kuku swadaqah; na mwenye kuondoka wakati wa saa ya tano kama ametoa yai swadaqah. Na Imamu anapojitokeza kutoa khutbah basi wakati huo Malaaika wanafika kusikiliza khutbah." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Hadiyth – 10

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ذَكَرَ يَوْمَ الجُمُعَةِ ، فَقَالَ : (( فِيهَا سَاعَةٌ لا يُوافِقُهَا عَبْدٌ مُسْلِمٌ ، وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي يَسْألُ اللهَ شَيْئاً ، إِلاَّ أعْطَاهُ إيّاهُ )) وَأشَارَ بيَدِهِ يُقَلِّلُهَا . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alieleza kuhusu siku ya Ijumaa akasema: "Ndani yake mna saa haafikiani nayo mja Muislamu akiwa anaswali na akimuomba kitu chochote Allaah isipokuwa atatimiziwa haja yake." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliashiria uchache au ufupi wa muda huo kwa mkono wake. [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 11

وعن أَبي بُرْدَةَ بن أَبي موسى الأشعريِّ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ عبد الله بن عمر رضي الله عنهما : أسَمِعْتَ أبَاكَ يُحَدِّثُ عَنْ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، في شأنِ سَاعَةِ الجُمُعَةِ ؟ قَالَ : قُلْتُ : نَعَمْ ، سَمِعْتُهُ يَقُولُ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( هِيَ مَا بَيْنَ أنْ يَجْلِسَ الإمَامُ إِلَى أنْ تُقْضَى الصَّلاةُ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Burdah bin Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa 'Abdullaah bin 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) alimuuliza: "Je, umemsikia babako akihadithia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu wakati ambao dua hukubaliwa?" Akasema: Nikasema: "Ndio, nimemsikia akisema: 'Ni wakati baina ya Imamu kukaa kwenye mimbari na kumalizika kwa Swalaah." [Muslim].

 

Hadiyth – 12

وعن أوس بن أوسٍ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ مِنْ أفْضَلِ أيَّامِكُمْ يَوْمَ الجُمُعَةِ ، فَأكْثِرُوا عَلَيَّ مِنَ الصَّلاَةِ فِيهِ ؛ فَإنَّ صَلاَتَكُمْ مَعْرُوضَةٌ عَلَيَّ )) رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .

Imepokewa kutoka kwa Aws bin Aws (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika miongoni mwa siku zenu, Ijumaa ndio siku bora, hivyo kithirisheni (ongezeni) kuniswalia ndani yake, kwani ninaonyeshwa Swalaah zenu hizo." [Abu Daawuwd, na Isnaad yake ni Swahiyh].

 

 

 

 

 

Share