05-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila ya Mtumwa Anayetekeleza Haki ya Allaah na ya Bwana Wake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب فضل المملوك الَّذِي يؤدي حق الله وحق مواليه

05-Mlango Wa Fadhila ya Mtumwa Anayetekeleza Haki ya Allaah na ya Bwana Wake

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( إنَّ العَبْدَ إِذَا نَصَحَ لِسَيِّدِهِ ، وَأَحْسَنَ عِبَادَةَ اللهِ ، فَلَهُ أَجْرُهُ مَرَّتَيْنِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika mtumwa anapomnasihi Bwana wake (anapomtumikia), na akafanya vizuri ibada ya Allaah, basi ana malipo mawili." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لِلْعَبْدِ المَمْلُوكِ المُصْلِحِ أجْرَانِ )) ، وَالَّذِي نَفْسُ أَبي هُرَيْرَةَ بِيَدِهِ لَوْلاَ الجِهَادُ في سَبيلِ اللهِ وَالحَجُّ ، وَبِرُّ أُمِّي ، لأَحْبَبْتُ أنْ أَمُوتَ وَأنَا مَمْلُوكٌ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtumwa mcha Mungu ana malipo mawili." Naapa kwa ambaye nafsi ya Abu Huraiyrah iko mkononi mwake, lau si Jihaadi katika njia ya Allaah na Hijjah na kumtendea wema mama yangu, basi ningependa nife nami ni mtumwa." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 3

عن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( المَمْلُوكُ الَّذِي يُحْسِنُ عِبَادَةَ رَبِّهِ ، وَيُؤَدِّي إِلَى سَيِّدِهِ الَّذِي عَلَيْهِ مِنَ الحَقِّ ، وَالنَّصِيحَةِ ، وَالطَّاعَةِ ، لهُ أجْرَانِ )) رواه البخاري .

Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtumwa anayefanya vyema ibada ya Rabb wake na kutekeleza haki ya bwana wake, na nasaha, na utii, ana malipo mawili." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( ثَلاثَةٌ لَهُمْ أجْرَانِ : رَجُلٌ مِنْ أَهْلِ الكِتَابِ آمَنَ بِنَبِيِّهِ ، وَآمَنَ بِمُحَمَّدٍ ، وَالعَبْدُ المَمْلُوكُ إِذَا أدَّى حَقَّ الله ،  وَحَقَّ مَوَالِيهِ ، وَرَجُلٌ كَانَتْ لَهُ أَمَةٌ فَأدَّبَهَا فَأَحْسَنَ تَأدِيبَهَا ، وَعَلَّمَهَا فَأَحْسَنَ تَعْلِيمَهَا ، ثُمَّ أعْتَقَهَا فَتَزَوَّجَهَا ؛ فَلَهُ أَجْرَانِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Watu aina tatu wana ujira mara mbili: Mtu miongoni mwa watu waliopewa Kitabu ambaye alimuamini Nabiy wake na kumuamini Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam); na mja ambaye ni mtumwa anayetekeleza haki ya Allaah na bwana wake; na mtu aliyekuwa na kijakazi, naye akampatia adabu iliyo mzuri na akamfundisha adabu kabisa, kisha akamuacha huru na kumuoa atakuwa na ujira mara mbili." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 
 
Share