006-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri: Kuapa Kwa Majina Na Sifa Za Allaah

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ

Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri

 

06- Kuapa Kwa Majina Na Sifa Za Allaah

 

Alhidaaya.com

 

 

[Al-Mughniy (11/182) na Al-Majmuw’u (18/22)].

 

Hakuna makhitalifiano yoyote kati ya ‘Ulamaa kuwa kiapo kinafungika kwa mwenye kusema "وَاللهِ" , au "بِاللهِ" , au "تَاللهِ" , na ni juu yake kafara kama atakivunja kiapo chake.  Na pia kinafungika kwa kuapa kwa Jina lolote kati ya Majina Yake Subhaanah Ambayo haitwi Kwayo mwingine yoyote isipokuwa Yeye tu kama [الرَّحْمنُ] “Ar-Rahmaan”, au  [الْأَوَّلُ الَّذِيْ لَيْسَ قَبْلَهُ شَيْءٌ] “Wa Mwanzo Ambaye hakuna kabla Yake kitu” , au [رَبُّ الْعَالَمِيْنَ] “Mola wa walimwengu”, au [الْحَيُّ الَّذِيْ لاَ يَمُوْتُ] “Aliye Hai Ambaye Hafi” , na mfano wa hayo.  

 

Ama majina ambayo huitwa kwayo asiye Allaah kwa majazi na ambayo pia hunasibishwa kwa Allaah Ta’aalaa kama الْخَالِقُ , الرَّزَّاقُ , الرَّبُّ , الرَّحِيْمُ , الْقَاهِرُ na mfano wake, haya yote huitwa kwayo asiye Allaah kwa majazi kwa ushahidi wa Neno Lake Ta’aalaa:

 

"وَتَخْلُقُونَ إِفْكًا"

 

“Na mnaunda uzushi”.  [Al-‘ Ankabuwt (29:17)].

 

Na Neno Lake:

 

"أَتَدْعُونَ بَعْلًا وَتَذَرُونَ أَحْسَنَ الْخَالِقِينَ"

 

“Mnamwomba (sanamu linaloitwa) ba-’alaa, na mnaacha Mbora wa wenye kuumba?".  [As-Swaaffaat (37:125)].

 

Na Neno Lake:

 

"ارْجِعْ إِلَىٰ رَبِّكَ"

 

“Rejea kwa bwana wako”.  [Yuwsuf (12:50)].

 

Na:

 

"اذْكُرْنِي عِندَ رَبِّكَ"

 

“Nikumbuke mbele ya bwana wako”[Yuwsuf (12:42)].

 

Majina haya ikiwa atakusudia kwayo Jina la Allaah au akajiropokea tu bila uainisho, basi kinakuwa ni kiapo, kwa kuwa kwa kuyataja, Yananasibika Kwake Allaah.  Na kama akikusudia asiye Allaah Ta’aalaa, basi haiwi kiapo, kwa kuwa yanatumika kwa wengineo.  Hivyo unasibisho wa majina haya kwa Allaah, utategemea niya ya mwapaji.

 

Ama majina ambayo anaitwa kwayo Allaah Ta’aalaa na wengineo na wala hayanasibiki Kwake tu kwa kuitwa kama aliye hai, mjuzi, mkarimu na mfano wake, haya, ikiwa atakusudia kwayo kuapa kwa Jina la Allaah Ta’aalaa, basi kiapo kinazingatiwa.  Na kama ataita au akakusudia asiye Allaah, basi hakizingatiwi.

                       

Share