007-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri: Kuapa Kwa Sifa Za Allaah Ta’aalaa

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ

Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri

 

07- Kuapa Kwa Sifa Za Allaah (تعالى)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

(a)  Kwa mujibu wa Jumhuwri  ya ‘Ulamaa, inajuzu kuapa kwa Sifa kati ya Sifa za Dhati ya Allaah Subhaanah ambazo hakusudiwi Kwazo mwingine Zaidi Yake Ta’aalaa kama Ujalali Wake, Kibri Chake, Uadhama Wake, na ‘Izzati Yake, na kiapo kinafungika Kwazo.

 

Toka kwa Anas amesema: Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) amesema:

 

"لاَ تَزَالُ جَهَنَّمُ تَقُولُ هَلْ مِنْ مَزِيدٍ حَتَّى يَضَعَ رَبُّ الْعِزَّةِ فِيهَا قَدَمَهُ فَتَقُولُ قَطْ قَطْ وَعِزَّتِكَ‏.‏ وَيُزْوَى بَعْضُهَا إِلَى بَعْضٍ"

 

“Jahannam itaendelea kusema: Je, kuna zaidi [watu kuja kuingia]?  Mpaka Rabbu wa ‘Izzah Atakapoweka ndani yake Mguu Wake, na hapo itasema: Inatosha, inatosha, naapa kwa ‘Izzati Yako.  Na sehemu zake zitakutanishwa zenyewe kwa zenyewe”.  [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6661) na Muslim (2848)].

 

Na katika Hadiyth ya Abu Hurayrah –katika kuelezea mtu wa mwisho atakayetoka motoni-,:

 

"فَلاَ يَزَالُ يَدْعُو اللَّهَ‏.‏ فَيَقُولُ لَعَلَّكَ إِنْ أَعْطَيْتُكَ أَنْ تَسْأَلَنِي غَيْرَهُ‏.‏ فَيَقُولُ لاَ وَعِزَّتِكَ لاَ أَسْأَلُكَ غَيْرَهُ"

 

“Na ataendelea kumwomba Allaah bila kuchoka.  [Allaah] Atamwambia: Je haiwezekani Nikikupa utaniomba jingine?  Atasema laa, naapa kwa Nguvu Zako zisizoshindika (‘Izzati Yako), sitokuomba jingine zaidi ya hilo”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6573) na Muslim (183)].

 

Na katika mapokezi ya Abu Hurayrah, Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) anasema:

 

"بَيْنَا أَيُّوبُ يَغْتَسِلُ عُرْيَانًا فَخَرَّ عَلَيْهِ جَرَادٌ مِنْ ذَهَبٍ، فَجَعَلَ أَيُّوبُ يَحْتَثِي فِي ثَوْبِهِ، فَنَادَاهُ رَبُّهُ يَا أَيُّوبُ، أَلَمْ أَكُنْ أَغْنَيْتُكَ عَمَّا تَرَى قَالَ بَلَى وَعِزَّتِكَ وَلَكِنْ لاَ غِنَى بِي عَنْ بَرَكَتِكَ"

 

“Wakati Ayyuwb alipokuwa anaoga uchi, nzige wa dhahabu walimwangukia. Ayyuwb akaanza kuwakusanya kwenye nguo zake.  Mola wake akamwita: Ee Ayyuwb!  Je, Sijakupa vya kutosha kiasi cha wewe kutowahitajia hivyo? Akasema: Na’am, naapa kwa ‘Izzati Yako, lakini siwezi kutosheka na Baraka Zako”.  [Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (279) na Muslim (2806)].

 

Na toka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) alikuwa anasema:

 

"أَعُوذُ بِعِزَّتِكَ الَّذِيْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ، الَّذِيْ لاَ يَمُوتُ وَالْجِنُّ وَالإِنْسُ يَمُوتُونَ"

 

“Najilinda kwa “Izzat Yako Ambaye hapana mwingine wa kuabudiwa isipokuwa Wewe tu, Ambaye Hafi, hali ya kuwa majini na wana wa Aadam wanakufa”.  [Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (7383) na Muslim (2717)].

 

Katika Hadiyth hii, kuna dalili kwamba inajuzu kujilinda kwa Sifa kati ya Sifa za Allaah, na pia katika kuapa, kwa kuwa yote mawili hayawi isipokuwa kwa Allaah tu.

 

(b)  Ama Sifa za Vitendo vya Allaah Ta’aalaa, hili tushaligusia nyuma katika Hadiyth ya Ibn ‘Umar isemayo: “Kiapo cha Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) kilikuwa:

 

"لاَ وَمُقَلِّبِ الْقُلُوبِ" ‏

 

“Laa, naapa kwa Mpinduaji wa nyoyo”.  [Hadiyth Swahiyh].

 

Ibn Al-’Arabiy (Rahimahul Laah) amesema:  “Katika Hadiyth hii, tunapata kuelewa kuwa inajuzu kuapa kwa Vitendo vya Allaah kama Atasifiwa Navyo bila kutaja Jina Lake.  Na kama mtu ataapa kwa Sifa kati ya Sifa Zake, au kwa Kitendo kati ya Vitendo Vyake bila uainisho, basi hakiwi ni kiapo kutokana na tuliyoyasema nyuma katika neno lake Rasuli:

 

"مَنْ كَانَ حَالِفًا فَلْيَحْلِفْ بِاللَّهِ أَوْ لِيَصْمُتْ"

 

“Mwenye kuapa, basi aape kwa Allaah, au anyamaze”.

 

Na kama akiapa kwa Sifa kati ya Sifa za Allaah, basi kinakuwa ni kiapo, na akikivunja, basi ni lazima atoe kafara.  Hivi hivi wamesema ‘Ulamaa wa Kimaalik na Kishaafi’iy toka kwa Maalik na Ash-Shaafi’iy mpaka enzi yetu ya leo”.  [‘Aaridhwat Al-Ahwaziy (7/23].

                                               

 

 

 

Share