08-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Chinjo La Kisharia: Kama Ikishindikana Kumdhibiti Mnyama Ili Kumchinja

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

 

 التَّذْكِيَةُ الشَّرْعِيَّةُ

 

Chinjo La Kisharia

 

 

Alhidaaya.com 

 

 

 

08-Chinjo La Kisharia: Kama Ikishindikana Kumdhibiti Mnyama Ili Kumchinja

 

[Al-Muhallaa (7/446), Naylul Awtwaar (8/163) na As Saylul Jarraar (4/68)]

 

 

Kama mchinjaji hakuweza kumdhibiti mnyama na ikawa ni vigumu kumchinja kwa kutoroka au mfano wa hivyo, hapo itajuzu kumchoma kwa chochote chenye ncha kali, au kumpiga mshale, au risasi na kadhalika katika sehemu yoyote ya mwili wake kiasi cha kuweza kumjeruhi na kumuua.  Kwa kufanya hivyo, nyama yake itakuwa ni halali kuliwa.  Na hii ndio kauli ya Jumhuwr ya ‘Ulamaa.  Lakini Maalik na Al-Layth hawalikubali hili!

 

Dalili ya Jumhuwr ni Hadiyth ya Raafi’u bin Khadiyj aliyesema:

 

 "كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سَفَرٍ ، فَنَدَّ بَعِيرٌ مِنْ إِبِلِ الْقَوْمِ ، وَلَمْ يَكُنْ مَعَهُمْ خَيْلٌ ، فَرَمَاهُ رَجُلٌ بِسَهْمٍ فَحَبَسَهُ ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ :‏ "‏إِنَّ لِهَذِهِ الْبَهَائِمِ أَوَابِدَ كَأَوَابِدِ الْوَحْشِ فَمَا فَعَلَ مِنْهَا هَذَا فَافْعَلُوا بِهِ هَكَذَا ‏"

 

 “Tulikuwa pamoja na Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) safarini. Ghafla, ngamia mmoja katika ngamia wa watu alichopoka na kukimbia, nao hawakuwa na farasi.  Mtu mmoja akampiga mshale (wa mguuni), ukamfanya asiweze tena kwenda.  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:  Hakika baadhi ya wanyama hawa (tuwafugao), wana tabia za ukali kama walivyo wanyama wakali, na kama atafanya yeyote kati yao tabia hizo, basi nanyi pia mfanyieni hivyo hivyo”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5543) na Muslim (1968)].

 

Na katika tamshi jingine,

 

"فَإِذَا غَلَبَكُمْ مِنْهَا شَىْءٌ فَاصْنَعُوا بِهِ هَكَذَا"

 

“Na kama atawashindeni nguvu, basi nanyi mtumilieni nguvu”.

                                                                       

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share