09-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Chinjo La Kisharia:Chinjo La Mama Ndilo Chinjo La Mtoto Aliye Tumboni Mwake

 

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

 

 التَّذْكِيَةُ الشَّرْعِيَّةُ

 

Chinjo La Kisharia

 

 

Alhidaaya.com 

 

 

 

09-Chinjo La Kisharia: Chinjo La Mama Ndilo Chinjo La Mtoto Aliye Tumboni Mwake

 

[Al-Majmuw’u (9/147), Naylul Awtwaar (8/164) na Subulus Salaam (4/1412)]

 

Mnyama akichinjwa kisha akatoka matumboni mwake kitoto kikiwa kimekufa, basi kwa mujibu wa kauli mbili zilizo sahihi zaidi za Jumhuwr, kitoto hicho ni halali kuliwa, kwani kinakuwa kimechinjwa kwa chinjo la mama yake.  Lakini Abu Haniyfah amekhitilafiana nao.

 

Kauli hii ya Jumhuwr inaungwa mkono na Hadiyth ya Abu Sa’iyd aliyesema: “Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu kitoto cha matumboni mwa mnyama.  Akasema:

 

"كُلُوْهُ إِنْ شِئْتُمْ"

 

“Kileni mkipenda”.

 

Na katika riwaayah nyingine:  Nilisema (Abu Sa’iyd):

 

"يَا رَسُولَ اللَّهِ ، نَنْحَرُ النَّاقَةَ وَنَذْبَحُ الْبَقَرَةَ وَالشَّاةَ فَنَجِدُ فِي بَطْنِهَا جَنِينا أَنُلْقِيهِ أَمْ نَأْكُلُهُ ؟ قَالَ: كُلُوهُ إِنْ شِئْتُمْ فَإِنَّ ذَكَاتَهُ ذَكَاةُ أُمِّهِ"

 

“Ee Rasuli wa Allaah!   Tunachinja ngamia, tunachinja ng’ombe na mbuzi, na tunakuta matumboni mwao kitoto.  Je, tukitupe au tukile?  Akasema:  Kileni mkipenda, kwani chinjo lake ni chinjo la mama yake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2827), At-Tirmidhiy (1476) na Ibn Maajah (3199)].

 

Lakini kama kitatoka kikiwa kizima na uhai kamili, basi hapo itakuwa si halali kukila ila kwa kukichinja.  Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.

 

                                               

 

 

 

 

 

 

 

 

Share