10-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Chinjo La Kisharia: Sehemu Ya Mnyama Iliyokatwa Akiwa Hai

 

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

 التَّذْكِيَةُ الشَّرْعِيَّةُ

 

Chinjo La Kisharia

 

Alhidaaya.com 

 

 

 

10- Chinjo La Kisharia: Sehemu Ya Mnyama Iliyokatwa Akiwa Hai

 

[Al-Muhallaa (7/449), Al-Mughniy (9/320) na Naylul Awtwaar (8/166)]

 

Toka kwa Abu Waaqid Al-Laythiy:  Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"مَا قُطِعَ مِنَ الْبَهِيمَةِ وَهِيَ حَيَّةٌ فَهُوَ مَيْتَةٌ"

 

“Chochote kilichokatwa kwa mnyama akiwa hai, basi kipande hicho ni mfu”. [Hadiyth Hasan.  Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2858), na At-Tirmidhiy (1480). Ina Hadiyth wenza].

 

Ibn Hazm (Rahimahul Laah] amesema:

 

“Sehemu yoyote iliyokatwa ya mnyama akiwa bado hai, au ikakatwa kabla ya kukamilika zoezi la kumchinja, basi sehemu hiyo ni mfu, si halali kuliwa.  Na kama kazi ya kumchinja itakamilika baada ya kukata sehemu hiyo, basi hapo mnyama ataliwa kama kawaida, lakini sehemu hiyo iliyokatwa haitofaa kuliwa. Na hili halina makhitilafiano kabisa, kwa kuwa kipande hicho kinakuwa kimetengana na mnyama ambaye ni haramu kumla (kabla ya kuchinjwa), na kinakuwa hakihusiani tena na chinjo litakalofanyika, kwani kinakuwa kiko nje ya asili yake”.  [Al-Muhallaa (7/449].

 

 

Share