003-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vinavyoruhusiwa Na Vinavyopendeza Zaidi Kuvaliwa Na Wanaume

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

 

 

اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ 

Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume 

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

003- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vinavyoruhusiwa Na Vinavyopendeza Zaidi Kuvaliwa Na Wanaume:

 

·        Nguo Nzuri Zaidi Ni Nyeupe

 

1-  Samurah:  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"الْبَسُوا مِنْ ثِيَابِكُمُ الْبَيَاضَ ، فَإِنَّهَا أَطْهَرُ وَأَطْيَبُ ، وَكَفِّنُوا فِيهَا مَوْتَاكُمْ"

 

“Vaeni katika nguo zenu zilizo nyeupe, kwani ndizo zenye utwahara zaidi na zilizo nzuri zaidi, na wakafinieni kwazo maiti wenu”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na An-Nasaaiy (4/8-34), Ibn Maajah (3567) na Ahmad (5/12,20)].

 

Na katika riwaayah: 

 

"عَلَيْكُمْ بِالْبَيَاضِ مِنَ الثِّيَابِ ، فَلْيَلْبَسْهَا أَحْيَاؤُكُمْ وَكَفِّنُوا فِيهَا مَوْتَاكُمْ ، فَإِنَّهَا مِنْ خَيْرِ ثِيَابِكُمْ" 

 

“Shikamaneni na nguo nyeupe, wazivae walio hai wenu na wakafinieni kwazo maiti wenu, kwani hizo ndizo nguo zenu zilizo bora zaidi”.

 

Ash-Shawkaaniy (Rahimahul Laah) amesema:  “Ama kuwa kwake zinapendeza zaidi, hilo liko wazi.  Ama kuwa kwake ni twaharifu zaidi, ni kwa kuwa zikipatwa na chochote hata kiwe kidogo, basi kitaonekana haraka na nguo itasafishwa, na kikiwa ni najisi, nguo itatwaharishwa.  Na amri tajwa katika Hadiyth si ya wajibu kutokana na yaliyothibiti toka kwake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba alivaa nguo za rangi nyingine.  Lakini pia, Maswahaba wengi walivaa nguo zisizo nyeupe, na Rasuli pia aliwakubalia Maswahaba wengi kuvaa nguo za rangi tofauti”.  [Naylul Awtwaar kwa marekebisho madogo].

 

2-  Sa’ad kasema:  

 

 "رَأَيْتُ بِشِمَالِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَبِيَمِينِهِ رَجُلَيْنِ عَلَيْهِمَا ثِيَابٌ بِيضٌ يَوْمَ أُحُدٍ، مَا رَأَيْتُهُمَا قَبْلُ وَلاَ بَعْدُ"

 

“Niliwaona kushotoni na kuliani mwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) watu wawili wenye nguo nyeupe Siku ya Uhud.  Sikuwahi kuwaona kabla (ya Siku hiyo) wala baada yake”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5826)].

 

3-  Abu Dharri amesema:

 

"أَتَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَعَلَيْهِ ثَوْبٌ أَبْيَضُ وَهُوَ نَائِمٌ"

 

“Nilimwendea Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), nikamkuta amelala akiwa amevaa nguo nyeupe”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5827)].

 

·        Hakuna Ubaya Kuvaa Nguo Isiyo Nyeupe

 

1-  Al-Baraa kasema: 

 

" كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَرْبُوعًا، وَقَدْ رَأَيْتُهُ فِي حُلَّةٍ حَمْرَاءَ مَا رَأَيْتُ شَيْئًا أَحْسَنَ مِنْهُ"

 

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na kimo cha wastani.  Niliwahi kumwona akiwa amevaa vazi jekundu la juu na chini, sijapata kuona kitu kizuri zaidi kuliko yeye.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5848).  Ina Hadiyth mwenza ya Jaabir iliyoko kwa At-Tirmidhiy (2811)].

 

2-   ‘Aaishah kasema:

 

"خَرَجَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ذَاتَ غَدَاةٍ وَعَلَيْهِ مِرْطٌ مُرَحَّلٌ مِنْ شَعَرٍ أَسْوَدَ "

 

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka asubuhi moja akiwa amevaa nguo ya chini (ya Yemen) ya sufi nyeusi yenye michoro ya kiti cha kukalia ngamia”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (2081), At-Tirmidhiy (2813) na Abu Daawuwd (402)].

 

3-  Qataadah amesema:

 

"قُلْنَا لأَنَسٍ: أَىُّ اللِّبَاسِ كَانَ أَحَبَّ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم؟ قَالَ: "الْحِبَرَةُ"

 

“Tulimuuliza Anas:  Ni kivazi gani alichokuwa akikipenda zaidi Rasuli wa Allaah?  Akasema:  Ni “Alhibarah”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5812) na Muslim (2081)].

 

“Alhibarah” ni vazi lenye marembo na mistari, hutengenezwa kwa kitani au sufi.

 

4-  Abu Rimthata amesema: 

 

"رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَخْطُبُ وَعَلَيْهِ بُرْدَانِ أَخْضَرَانِ" 

 

“Nilimwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anakhutubu akiwa amevaa vishali viwili vya kijani”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (2813), Abu Daawuwd (4206), An-Nasaaiy (8/204) na Ahmad (2/227)].

 

5-  Vazi la kijani litavaliwa zaidi na watu wa Peponi.  Allaah Ta’aalaa Amesema:  

 

"عَالِيَهُمْ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضْر"

 

“Watavaa nguo za hariri nyororo za kijani”.  [Al-Insaan: 21].

 

                                                

 

 

 

 

 

 

Share