016-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume:Wanaume Kujipaka Wanja

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

 

اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ 

Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume 

 

Alhidaaya.com 

 

 

 

 

016-  Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume:  Wanaume Kujipaka Wanja:

 

 

Hakuna ubaya kwa wanaume kupaka wanja ikiwa ni kwa ajili ya kuimarisha nguvu ya kuona, kuondosha utando wa jicho, kulisafisha na kulitwaharisha, au kwa ajili ya tiba, na hususan ikiwa ni kwa wanja asili wa “Al-Ithmid”.  Na hii ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

"وَإِنَّ خَيْرَ أَكْحَالِكُمُ الإِثْمِدُ، يَجْلُو الْبَصَرَ، وَيُنْبِتُ الشَّعْرَ‏"

 

“Na hakika wanja wenu ulio bora zaidi ni wa “ithmid”, unasafisha macho, unaotesha kope”.  [Hadiyth Hasan.  Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3878), At-Tirmidhiy (994), An-Nasaaiy (8/15) na Ibn Maajah (3497)].

 

Ama kutia wanja kwa ajili ya kujipamba na kujitengeneza, kwa hili, hakuna Hadiyth yoyote iliyothibiti.  Imesimuliwa kwamba:  “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitia wanja kwenye jicho lake la kulia mara tatu, na la kushoto mara mbili”.  Lakini Hadiyth hii haikuthibiti.

 

Inavyoonekana ni kwamba si katika Sunnah kama wanavyoitakidi watu wengi.

 

Al-‘Allaamah Ibn ‘Uthaymiyn amesema:  “Ama wanaume, hapo ni pa kutafitiwa zaidi, na mimi siko huku wala kule.  Lakini hata hivyo, suala hili linaweza kupambanuliwa kati ya kijana ambaye inahofiwa fitna kama atajipaka, huyu haruhusiwi, na kati ya mtu mzima ambaye hahofiwi lolote, huyu hakatazwi”.  [Fataawaa Ziynatil Mar-at wat-Tajmiyl (uk.51)].

 

Ninasema:  “Ama kwa mwanamke, hili linatakiwa na hususan kujipamba kwa ajili ya mumewe”.  

 

Share