104-Al-Humazah: Utangulizi Wa Suwrah

 

104-Al-Humazah: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

Imeteremka: Makkah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.

 

Idadi Za Aayah: 9

 

Jina La Suwrah: Al-Humazah

 

Suwrah imeitwa Al-Humazah (Kufedhehesha, Kukashifu Kwa Ishara Na Vitendo), na inayodalilisha ni kutajwa kwake katika Aayah namba (1).

 

Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:

 

1-Kuwatahadharisha wanaadam juu ya kuwafanyia istihzai Waumini kwa kudanganyika kwao na uwingi wa mali. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]

 

2-Kutaja sifa za wenye kuangamia.

 

Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:

 

Suwrah imefunguliwa kwa ahadi ya kuadhibiwa kila mwenye kwavunjia watu heshima zao kwa kukawakshifu, kuwadharau, kukebehi na kadhaalika kwa ishara na vitendo. Na pia kila mwenye kusengenya, kukashifu na kadhaalika kwa ulimi. Na sifa ya mtu huyo ni yule anayerundika mali na kupenda kuhesabu, wala hana raghba ya kuitolea mali katika Aliyoyaamrisha Allaah (سبحانه وتعالى) kama Zakaah na swadaqa, au kuwagaiya arhaam (wenye uhusiano wa damu), na mengineyo ya khayraat. Basi anadhania kwamba mali yake ambayo ameikusanya, inampa dhamana ya kuishi milele duniani na itamfanya akwepe kuhesabiwa. Lakini anayoyadhania siyo kabisa! Kwani bila shaka ataingiziwa katika moto ulio na sifa ya Hutwamah, yaani moto unavunjavunja kila kinachotupwa humo. Na kwa ukali wa moto huo, unapenya miilini ukafika nyoyoni. Na umefunga milango yake baada ya kutumbukizwa watu humo kwenye nguzo ndefu ili wasiweze kutoka kamwe!

 

 

Share