02-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Mwanaume Anaruhusiwa Kumwangalia Mwanamke Kwa Ajili Ya Maslaha Mazito

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com 

 

 

02-Mwanaume Anaruhusiwa Kumwangalia Mwanamke Kwa Ajili Ya Maslaha Mazito:

 

Tumeshajua kwamba mwanaume kumwangalia mwanamke -na kinyume chake- ni haramu, kwa kuwa kuangalia ni njia na sababu ya kupelekea kufanyika machafu.  Lakini kuangalia huku kunaruhusiwa endapo kama kuna maslaha mazito.  Na hii ni kutokana na Hadiyth ya ‘Aliyy kuhusiana na kisa cha yeye pamoja na Az-Zubayr na Abu Marthad kutumwa na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwenda kumwahi mwanamke wa kipagani ambaye alikuwa na barua ya Haatib bin Balta’ah akiipeleka kwa wapagani wa Makkah.  Sehemu ya Hadiyth inasema:

 

"لَقَدْ عَلِمْتُ مَا كَذَبَ رَسُوْلُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، وَالَّذِي يُحْلَفُ بِهِ لَتُخْرِجِنَّ الْكِتَابَ أَوْ لَأُجَرِّدَنَّكِ ، فَأَهْوَتْ بِيَدِهَا إِلَى حُجْزَتِهَا فَأَخْرَجَتِ الْكِتَابَ "

 

“Kwa hakika ninajua kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakusema uongo.  Basi naapa kwa Yule Ambaye Huapiwa kwa Jina Lake, ima utaitoa barua, au nitakuvua nguo zote.  Akapeleka mkono kwenye fundo la nguo yake, akaitoa barua”.  [Al-Bukhaariy (3081) na Muslim (2494)]

 

Al-Haafidh amesema kwenye Al-Fat-h (11/47):  “Hadiyth inatufunza kwamba inajuzu kuangalia uchi wa mwanamke kwa dharura isiyo na budi”.

 

 

 

Share