05-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Mwanaume Kubisha Hodi Ili Kuingia Kwa Maharimu Zake

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com 

 

 

05-Mwanaume Kubisha Hodi Ili Kuingia Kwa Maharimu Zake:

 

Nyuma pamekwisha ainishwa uchi wa mwanamke mbele ya maharimu zake, na kwamba mwanamke haamuriwi kujifunika mbele ya maharimu hawa.  Lakini pamoja na hivyo, haitakikani mwanamume aingie kwa maharimu zake bila kuwabishia, kwani anaweza kuingia bila hodi akawakuta katika hali isiyofurahisha, kama kuwa uchi na mfano wa hivyo.

 

‘Alqamah amesema:  “Mtu mmoja alikwenda kwa ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd akamwambia: 

 

"أأَسْتَأْذِنُ عَلَى أُمِّيْ؟ قَالَ: مَا عَلَى كُلِّ أَحْيَانِهَا تُحِبُّ أَنْ تَرَاهَا"

 

“Je, nipige hodi kuingia kwa mama yangu?  Akamwambia:  Si katika nyakati zake zote anapenda umwone”.  [Al-Bukhaariy katika Al-Adab Al-Mufrad (1059) kwa Sanad Swahiyh]

 

‘Atwaa amesema:  “Nilimuuliza Ibn ‘Abbaas:  

 

"أَسْتَأْذِنُ عَلَى أُخْتَىّْ؟  فَفَالَ: نَعَمْ فَقُلْتُ: أُخْتَانِ في حِجْرِيْ وأَنا أُمَوِّنُهُمَا وأُنْفِقُ عَلَيْهِمَا، أَسْتَأْذِنُ عَلَيْهِمَا؟ قَالَ: نَعَمْ، أَتُحِبُّ أَنْ تَرَاهُمَا عرْيَانَتَيْنِ؟!"

 

“Je, nipige hodi kuingia kwa dada zangu?  Akasema:  Na’am.  Nikamwambia:  Hao ni dada zangu wawili ninawalea, na mimi ndiye ninawakimu kimaisha na kuwapa masurufu, vipi niwabishie?!  Akasema:  Na’am.  Je, utapenda kuwaona wakiwa uchi?!  Kisha akasoma:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لِيَسْتَأْذِنكُمُ الَّذِينَ مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ وَالَّذِينَ لَمْ يَبْلُغُوا الْحُلُمَ مِنكُمْ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ ۚ مِّن قَبْلِ صَلَاةِ الْفَجْرِ وَحِينَ تَضَعُونَ ثِيَابَكُم مِّنَ الظَّهِيرَةِ وَمِن بَعْدِ صَلَاةِ الْعِشَاءِ ۚ ثَلَاثُ عَوْرَاتٍ لَّكُمْ ۚ

 

“Enyi walioamini!  Wakuombeni idhini wale iliyowamiliki mikono yenu ya kuume, na wale wasiofikia umri wa kubaleghe miongoni mwenu mara tatu: kabla ya Swalaah ya alfajiri na wakati mnapovua nguo zenu adhuhuri (kulala) na baada ya Swalaah ya ‘Ishaa.  Nyakati tatu za faragha kwenu”.  [Al-Bukhaariy katika Al-Adab Al-Mufrad (1063) kwa Sanad Swahiyh]

 

 

 

Share