06-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Ni Haramu Kwa Mwanaume Kukaa Pweke na Mwanamke Asiye Maharimu Yake (Ajnabiyyah)

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com 

 

 

06-Ni Haramu Kwa Mwanaume Kukaa Pweke na Mwanamke Asiye Maharimu Yake (Ajnabiyyah):

 

 

Ibn ‘Abbaas:  “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: 

 

"لاَ يَخْلُوَنَّ رَجُلٌ بِامْرَأَةٍ إِلاَّ وَمَعَهَا ذُو مَحْرَمٍ ‏"

 

“Mwanaume kamwe asibaki pweke na mwanamke ila akiwa pamoja naye mahram yake”. [Al-Bukhaariy 3006) na Muslim (1341]

 

Na Rasuli anasema tena:

 

"لَا يَخْلُوَنَّ رَجُلٌ بِامْرَأَةٍ، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ ثَالثُهُمَا"

 

“Kamwe asibaki mwanaume pweke na mwanamke, kwani shaytwan atakuwa ni wa tatu wao”.  [Ahmad katika Al-Musnad (1/18) kwa Sanad Swahiyh]

 

Na ikiwa wanaume wawili au watatu ambao wanaaminika na uwezekano wa wao kula njama ya kufanya machafu uko mbali, basi wanaruhusiwa kuingia kwa mwanamke mmoja.  Na hii ni kwa Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Amri:

 

 "أَنَّ نَفَرًا مِنْ بَنِي هَاشِمٍ دَخَلُوا عَلَى أَسْمَاءَ بِنْتِ عُمَيْسٍ فَدَخَلَ أَبُو بَكْرٍ الصِّدِّيقُ وَهِيَ تَحْتَهُ يَوْمَئِذٍ  فَكَرِهَ ذَلِكَ ، فَذَكَرَ ذَلِكَ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَقَالَ: لَمْ أَرَ إِلاَّ خَيْرًا ‏.‏ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ‏"‏إِنَّ اللَّهَ قَدْ بَرَّأَهَا مِنْ ذَلِكَ"‏ ‏.‏ ثُمَّ قَامَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى الْمِنْبَرِ فَقَالَ: ‏"‏لاَ يَدْخُلَنَّ رَجُلٌ بَعْدَ يَوْمِي هَذَا عَلَى مُغِيبَةٍ إِلاَّ وَمَعَهُ رَجُلٌ أَوِ اثْنَانِ" 

 

“Watu kadhaa wa ukoo wa Bani Hashim waliingia kwa Asmaa bint ‘Umays.  Abu Bakr As-Swiddiyq akaingia -na Asmaa ashakuwa mkewe wakati huo- na jambo hilo halikumfurahisha.  Akaenda kumweleza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) lakini alimwambia:  Sikuona ila kheri (simtuhumu ubaya wala siwatuhumu).  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:  Hakika Allaah Amemtakasa na hilo.  Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasimama juu ya mimbari akasema:  Asiingie mwanaume yeyote baada ya siku hii kwa mwanamke ambaye mumewe hayuko ila awe pamoja naye mwanaume mwingine au wawili”.  [Swahiyh Muslim (2173)]

 

Vile vile, mwanaume anaruhusiwa kumzuru mwanamke mgonjwa kama ipo dhamana ya kutokuweko fitnah.   Na hii ni kwa Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdillaah aliyesema:

 

"أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ دَخَلَ عَلَى أُمِّ السَّائِبِ فَقَالَ: ‏"‏مَا لَكِ يَا أُمَّ السَّائِبِ، تُزَفْزِفِينَ"‏‏.‏ قَالَتِ: الْحُمَّى لاَ بَارَكَ اللَّهُ فِيهَا.‏ فَقَالَ: ‏"‏لاَ تَسُبِّي الْحُمَّى فَإِنَّهَا تُذْهِبُ خَطَايَا بَنِي آدَمَ كَمَا يُذْهِبُ الْكِيرُ خَبَثَ الْحَدِيدِ "

 

“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia kwa Ummu As-Saaib na kumwambia:  Una nini Ummu As-Saaib?  Naona unatetema.  Akasema:  Ni homa, Allaah Asiibariki.  Rasuli akamwambia:  Usiitukane homa, kwani homa inaondosha madhambi ya mwanadamu kama moto wa mfua chuma unavyosafisha uchafu wa chuma”.   

 

 

Share