09-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Mwanamke Haruhusiwi Kupeana Mkono Na Mwanaume Ajinabi (Asiye Maharimu)

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

 

  

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com 

 

 

 

09-Mwanamke Haruhusiwi Kupeana Mkono Na Mwanaume Ajinabi (Asiye Maharimu):

 

Ni kwa Hadiyth ya Mu’aql bin Yasaar:

 

"لأَنْ يُطْعَنَ فِي رَأْسِ أَحَدِكُمْ بِمِخْيَطٍ مِنْ حَدِيْدٍ خَيْرٌ لَهُ مِنْ أَنْ يَمَسَّ امْرَأَةً لا تَحِلُّ لَهُ"

 

“Kupondwa mmoja wenu kwa sindano la chuma, ni nafuu zaidi kuliko kumgusa mwanamke ambaye si halali kwake”.  [At-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr (20/211) kwa Sanad Hasan.  Angalia As-Silsilat As-Swahiyhah].

 

Kadhalika, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa akiwapa mkono wanawake, na wala hakuchukua kwao ahadi ila kwa maneno tu.

 

‘Aaishah anasema: 

 

"أَنَّ رَسُولَ الله صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَقُولُ للمَرْأَةِ المُبَايِعَةِ: "قَدْ بَايَعْتُكِ كَلَامًا"

 

“Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akimwambia mwanamke anayechukua kutoka kwake ahadi:  “Nimechukua ahadi toka kwako kwa maneno”. 

 

Pia anasema tena: 

 

وَاللَّهِ مَا مَسَّتْ يَدُهُ يَدَ امْرَأَةٍ قَطُّ فِي الْمُبَايَعَةِ، وَمَا بَايَعَهُنَّ إِلاَّ بِقَوْلِهِ‏:"قَدْ بَا يَعْتُكِ عَلى ذلِكَ"

 

“Wa-Allaah, mkono wake haujagusa kamwe mkono wa mwanamke katika kupeana nao ahadi.  Hakupeana nao ahadi ila kwa kuwaambia:  “Nimechukua ahadi kwako juu ya hilo”.   [Swahiyhul Bukhaariy (2713)].

 

Na katika riwaayah, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaambia:

 

"إِنِّيْ لَا أُصَافِحُ النِّسَاءَ ...."

 

 “Mimi sipeani mikono na wanawake”.  [Muwattwaa Maalik (1842), Ahmad (6/357), At-Tirmidhiy (1597), An-Nasaaiy (4181) na Ibn Maajah (2874)].

 

 

Share