04-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Kuweka Mkono Wako Juu Ya Kichwa Cha Mkeo Na Kumuombea

Inampasa mume, wakati wa kufunga ndoa na mkewe na kabla hajamuingilia, kuweka mkono wake juu ya kichwa chake (sehemu ya utosini), na kutaja jina la Allaah سبحانه وتعالى na kuomba Baraka za Allaah سبحانه وتعالى kama katika kauli ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم:

 

 ((إذَا تَزَوَّجَ أَحَدُكُمْ امْرَأَةً أَوْ اشْتَرَى خَادِماً ، [فليأخذ بناصيتها]  [وليسم الله عز وجل]،  فَلْيَقُلْ: اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ خَيْرَهَا وَخَيْرَ ما جَبَلْتَهَا عَلَيْهِ، وأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّهَا وَمِنْ شَرِّ مَا جَبَلْتَهَا عَلَيْهِ)) 

((Anapofunga ndoa mmoja wenu na mwanamke au anapomuajiri mfanyakazi basi amuekee mkono katika kipaji cha uso wake ataje jina la Allaah utosini mwake na kusema “Ee Allaah hakika mimi nakuomba kheri ya (mke) huyu na khayr uliyomuumbiya na najilinda Kwako na shari yake, na shari ya Uliyomuumbiya))[1]

 

 

[1] Al-Bukhaariy katika "Af'aalul-'ibaad", Abu Daawuud, Ibn Maajah, Al-Haakim, Al-Bayhaaqiy na Abuu Ya'alaa ikiwa ni isnaad hasan

Share