05-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Kuswali Mume Na Mke Pamoja

Inapendekezwa mume na mke kuswali Raka'ah mbili pamoja usiku wa ndoa yao. Hii imehadithiwa kutoka kizazi cha mwanzo cha Waislamu (Salafus Swaalih) kama katika masimulizi mawili yafuatayo:

Kwanza:

 

تزوجت وأنا مملوك، فدعوت نفراً من أصحاب النبي صلى الله عليه وسلم فيهم ابن مسعود وأبو ذر وحذيفة، قال: وأقيمت الصلاة، قال: فذهب أبو ذر ليتقدم، فقالوا: إليك! قال: أو كذلك؟ قالوا: نعم، قال: فتقدمت بهم وأنا عبد مملوك، وعلموني فقالوا:  إذا دخل عليك أهلك فصل ركعتين، ثم سل الله من خير ما دخل عليك، وتعوذ به من شره، ثم شأنك وشأن أهلك. 

 

Imetoka kwa Abu Sa'iyd Mawla Abu Asyad ambaye amesema: "Nilioa wakati nilipokuwa mtumwa. Nikaalika baadhi ya Maswahaba wa Mtume miongoni wao alikuwa Ibn Mas'uud, Abu Dharr na Hudhayfah. Adhaan ya Swalah iliponadiwa, Abu Dharr alianza kusogea mbele na wengine wakamwambia: Hapana! Akasema: 'Ni hivyo?' (Yaani nisiswalishe?) Wakasema: 'Ndio. Kisha nikasogea mbele na kuswalisha ingawa nilikuwa mtumwa niliyemilikiwa. Wakanifundisha kwa kusema: 'Atakapokujia mkeo, swali Raka'ah mbili kisha muombe kheri ya kile kilichokujia na jikinge kwake kutokana na shari yake. Kisha ni khiari yako na khiari ya mkeo"[1]

Pili:

 

 عن شقيق أنه قال:  جاء رجل يقال له: أبو حريز فقال: إني تزوجت جارية بكراً، وإني خشيت أن تَفْرَكَنِي، فقال عبد الله: أَلاَ إِنَّ إلالْفَ مِنَ الله وَإِن الفَرك مِنَ الشَّيْطان ليكره إليه ما أحل الله له، فإذا دخلت عليها، فمرها فلتصل خلفك ركعتين.( زاد في رواية أخرى عن ابن مسعود): اللهمَّ بَارِكْ لِي فِي أَهْلِي وَبَارِكْ لَهُمْ فِيَّ، اللَّهُمَّ ارزقهم مني وارزقني منهم، اللَّهم اجمعْ بيننا ما جمعت إلى خير، وفرِّق بيننا إذا فرقت إلى خير.

Imetoka kwa Shaqiyq ambaye amesema: "Mtu mmoja aliyeitwa Abu Hariyz alikuja na akasema: 'Nimeoa msichana mdogo na nakhofu kuwa atanibughudhi (atanitweza), 'Abdullaah Ibn Mas'uud akaniambia: 'Hakika upole (ukaribu) ni kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى na uhasama (chuki) ni kutoka kwa Shaytwaan ambaye anapenda kukuchukizeni (kuhizi) yale Aliyoyaruhusu Allaah سبحانه وتعالى. Kwa hiyo, mkeo atakapokuja kwako, mwambie aswali nyuma yako Raka'ah mbili'. (katika riwaaya nyingine ya masimulizi hayo hayo, 'Abdullaah aliendelea kusema) ((Ee Allaah, Nibarikie mke wangu, na Mbariki yeye kwangu. Ee Allaah Waruzuku kwangu na Niruzuku Kwao. Ee Allaah Tuunge pamoja madamu Utatuunga katika khayr na Tufarikishe (tuwe mbali mbali) Utakapotupeleka kwa yaliyo bora))[2]

 

 

 

[1] Ibn Abi Shaybah na 'Abdur-Razzaaq

[2] Ibn Abi Shaybah, At-Twabaraaniy na 'Abdur-Razzaaq: Swahiyh

Share