27-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Sunnah Ya Waliymah (Karamu)

Yafuatayo yanapaswa kutekelezwa katika karamu ya ndoa:

Kwanza:

Ifanyike siku tatu baada ya usiku wa ndoa kwani hii ndio desturi ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم iliyotufikia.[1]

 

 

فَعَنْ أَنَسْ رَضِيَ الله عَنْهُ قال:  بَنَى رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم  بِاِمْرَأةٍ، فَأَرْسَلَنيِ فَدَعَوْتُ رِجَالاً عَلىَ الطَّعَام 

Imetoka kwa Anas ambaye amesema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alipofunga ndoa aliniita ili nialike baadhi ya wanaume kuja kula chakula"[2]

 

 
Vile vile imetoka kwa Anas ambaye amesema:

 

تزوَّج رسولُ الله صلى الله عليه وسلّم صفيَّة، وجعل عَتْقَها صَدَاقَها، وجعل الوليمةَ ثلاثةَ أيَّامٍ، وبَسَط نِطعاً جاءت به أمُّ سُليم، وألقى عليه أَقِطاً وتَمراً، وأطعمَ النَّاسَ ثلاثةَ أيَّامٍ

 

"Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alimuoa Swafiyah na uhuru wake ndio ulikuwa mahari yake. Alifanya karamu kwa muda wa siku tatu"[3]

 

Pili:

Inapasa kuwaalika watu wema katika karamu yake ikiwa ni matajiri au maskini.

 

عن أَبي سَعِيدٍ، أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ الله يقولُ: ((لا تُصَاحِبْ إِلاَّ مُؤْمِناً وَلاَ يَأْكُلْ طَعَامَكَ إِلاَّ تَقِيٌ))

Kutoka kwa Sa'iyd kwamba amemsikia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akisema: ((Msiwe marafiki wa wowote isipokuwa waumini na wale chakula chenu watu wema pekee))[4]

 

 

Tatu:

Ikiwa mtu ana uwezo, afanye karamu ya kondoo mmoja au zaidi kutokana na Hadiyth ifuatayo:

 

عَنْ أَنَسْ رضي الله عنه قال: إِنَّ عَبْدُ الرَّحْمن بِنْ عَوْف قَدِمَ الْمَدِينَةَ  فآخى  رسولُ اللَّهِ بَيْنَهُ وبَيْنَ سَعْدِ بنِ الرَّبيعِ الأَنْصََارِي [فَانْطَلَقَ بِِهِ سَعَدْ إِلَى مَنْزِلِهِ، فَدَعَا بِطَعَام فأَكلَا]، فقال له سعد: أي أخي! أنا أكثر أهل المدينة ( وفي رواية: أكثر الأنصار )مالاً، فانظر شطر مالي فخذه ( وفي رواية: هلم إلى حديقتي أشاطركها  (، وتحتي امرأتان [وأنت أخي في الله  لا امرأة لك]، فانظر أيهما أعجب إليك [فسمها لي] حتى أطلقها [لك] [فإذا انقضت عدتها فتزوجها]، فقال عبد الرحمن: [لا والله]، بارك الله لك في أهلك ومالك، دلوني على السوق، فدلوه على السوق، فذهب، فاشترى وباع، وربح، [ثم تابع الغدو] فجاء بشيء من أقِطٍ- لبن مجفف يابس مستجر يطبخ به- وسمن [قد أفضله] [فأتى به أهل منزله]، ثم لبث ما شاء الله أن يلبث، فجاء وعليه ردع زعفران ( وفي رواية: وضر من خلوق )، فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم :(( مهْيَم؟)) فقال: يا رسول الله! تزوجت امرأة [من الأنصار]، فقال ((ما أصدقتها؟)) قال: وزن نواة من ذهب، قال: ((فبارك الله لك )) أولم ولو بشاة، [فأجاز ذلك]. قال عبد الرحمن: فلقد رأيتني ولو رفعت حجراً لرجوت أن أصيب [تحته] [ذهباً أو فضة]، [قال أنس: لقد رأيته قُسِم لكل أمرأة من نسائه بعد موته مائة ألف دينار]  ))

Anas amesema: "'Abdur-Rahmaan bin ‘Awf alikuja Madiynah na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akajengea udugu pamoja na Sa'ad ibn Ar-Rabiy' Al-Answaariy. Sa'ad alimchukua nyumbani kwake, akaagiza chakula na wakala pamoja. Kisha Sa'ad akasema: 'Ee ndugu yangu, mimi ni tajiri mkubwa kabisa katika watu wa Madiynah (katika riwaaya nyingine: "Katika Answaar" basi tazama nusu ya mali yangu na uchukue (katika riwaaya nyingine: 'Na nitagawa bustani yangu nusu). Pia ninao wake wawili (ilhali ndugu yangu kwa Allaah huna mke) basi mtazame yupi katika hao wangu aliyekupendeza zaidi ili nimpe talaka kwa ajili yako. Kisha baada ya kumalizika wakati wake wa kusubiri wa sheria (eda ya talaka) unaweza kumuoa. 'Abdur-Rahmaan akasema: 'Hapana Wa-Allaahi, Allaah Akubariki katika ahli na mali yako. Nionyeshe lilipo soko'. Akaonyeshwa njia ya sokoni akaenda huko. Akanunua na kuuza na kupata faida. Ilipofika jioni, alirudi kwa watu wake wa nyumbani akiwa na maziwa makavu ya kupikia na samli. Baada ya hapo siku zikapita hata akatokea siku moja na alama za zaafarani katika nguo yake. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akauliza, ((Kitu gani hiki?)) Akasema: 'Ee Mjumbe wa Allaah, nimeoa mwanamke miongoni mwa wanawake wa ki-Answaar. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  akauliza: ((Umempa nini mahari yake?)) Akasema: 'Abdur-Rahmaan akajibu, 'Dhahabu ya uzito wa dirham tano'.  Kisha Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema, ((Allaah Akubariki. Fanya karamu japo ya kondoo mmoja)) 'Abdur-Rahman akasema: 'Nilijiona niko katika hali ya kwamba ningelinyanyua jiwe lolote, ningetegemea kupata dhahabu au fedha chini yake'. Anas anasema: "Niliona baada ya mauti yake kila mke wake alirithi Dinari laki moja"[5]

 

 

  عَنْ أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ ، يَقُولُ:  مَا رَأَيْت رَسُولُ الله صَلى الله عليه وسلم أَوْلَمَ عَلَى امْرَأَةْ مِنْ نِسَائِهِ مَا أَوْلَمَ عَلىَ زَيْنَبْ، فَإنَّهُ ذَبَحَ شَاة، [قَالَ: أَطْعَمَهُمْ خُبْزاً وَلَحْماً حَتىَّ تَرَكُوه]  

Vile vile kutoka kwa Anas ambaye amesema: "Sijapata kumuona Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akifanya karamu kubwa kama karamu ya ndoa kama aliyofanya kwa Zaynab. Alichinja kondoo na kulisha watu wote nyama na mikate mpaka wakashiba"[6]

 

 

[1] Fat-hul Baariy 9/242-244

[2] Al-Bukhaariy na Al-Bayhaaqiy

[3] Abu Ya'laa na wengine: Hasan

[4] Abu Daawuud, At-Tirmidhiy na wengineo: Swahiyh

[5] Al-Bukhaariy, An-Nasaaiy na wengineo

[6] Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo

Share