30-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Makatazo Ya Kualika Matajiri Pekee

 

 

Hairuhusiwi kualika matajiri pekee na kuwatenga masikini kwani Mtume صلى الله عليه وآله وسلم   amesema:

 

 

((شَرُّ الطَّعَامِ طَعَامُ الْوَلِيمَةِ يُدْعَىٰ لَهَا الأَغْنِيَاءُ وَيُتْرَكُ الْمَسَاكِينُ، وَمَنْ لَمْ يَجِبْ الدَّعْوَةَ فَقَدْ عَصَىٰ اللَّهَ وَرَسُولَهُ)).

 

((Chakula kiovu kibaya kabisa ni chakula cha karamu ya harusi ambayo wamealikwa matajiri na kutengwa kando masikini. Yeyote atakayekataa mualiko atakuwa amemuasi Allaah na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Wake))[1]

 

[1] Muslim na Al-Bayhaaqiy

Share