31-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Ni Wajibu Kuitikia Mwaliko

 

 

Ni wajibu kwa anayealikwa karamu kuhudhuria. Kuna Hadiyth mbali mbali kuhusu jambo hili, miongoni mwa hizo ni:

 


Kwanza:

  ((فُكُّوا الْعَانِيَ، وَأَجِيبُوا الدَّاعِيَ، وَعُودُوا الْمَرِيضَ))

((Acheni huru wafungwa, itikieni (kubalini) mwaliko na tembeleeni wagonjwa))[1]

 



Pili:

 

((إِذَا دُعِيَ أَحَدُكُمْ إِلَى الْوَلِيمَةِ فَلْيَأْتِهَا  عَرْساً كَان أَوْ نَحْوه  وَمَنْ لَمْ يُجِبِ الدَّعْوَةَ، فَقَدْ عَصَى اللّهَ وَرَسُولَهُ))




((Anapoalikwa mmoja wenu katika karamu, basi ahudhurie, ikiwa ni karamu ya harusi au nyingineyo. Na yeyote asiyeitikia (asiyekubali) mwaliko basi atakuwa amemuasi Allaah na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Wake))[2]

 



[1] Al-Bukhaariy

[2] Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo

Share