37-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Kuwaombea Bwana Harusi Na Bibi Harusi Watoto Wengi (Wa Kiume) Ni Msemo Katika Ada Ya Ujahiliya (Kabla Ya Uislam)

 

 

Haipasi kusema "Ujaaliwe watoto wengi wa kiume" kama wanavyofanya wengi walio wajinga katika jamii nyingi, kwa sababu ni ada/mila ya watu wa kabla ya Uislamu katika zama za ujinga (Ujaahiliyyah) ambayo imeharamishwa katika Hadiyth zaidi ya moja.

عَنِ الْحَسَنِ  قَالَ: تَزَوَّجَ عَقِيلُ بْنُ أَبِي طَالِبٍ امْرَأَةً مِنْ بَنِي جَثمٍ  فدخل عليه القوم، فقالوا     "بِالرِّفَاءِ وَالْبَنِينِ"  فقَالَ: لا تفعلوا ذلك [فإن رسول الله صلى الله عليه وسلم نهى عن ذلك]، قَالُوا فَمَا نَقُول يآ أبا زَيْد؟ قَال:  قُولُوا( كَمَا قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم): ((بَارَكَ اللَّهُ فِيكُمْ وَبَارَكَ لَكُمْ)). ( إنا كذلك كنا نؤمر)

Imetoka kwa Al-Hasan رضي الله عنه kwamba 'Uqayl ibn Abi Twaalib alimuoa mwanamke kutoka kabila la Jathm. Watu walikuja nyumbani kwake na wakasema: "Ujaaliwe kupata watoto wengi wa kiume". 'Uqayl akawaambia: 'Msifanye hivyo, kwani Mtumeصلى الله عليه وآله وسلم amekataza hivyo'. Wakasema: Sasa tuseme nini ewe Abu Zayd? Akasema: Semeni kama alivyosema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم   ((Allaah Akubariki na Ateremshe Baraka juu yenu)). (Hivyo ndivyo tulivyoamrishwa kusema)"[1]

 

 

 



[1] Ibn Abi Shaybah, An-Nasaaiy na wengineo – yenye kutiliwa nguvu

Share