11-Uswuul Al-Fiqhi: Sifa Mahsusi Za Fiqhi Wakati Huo

 

 

a.      Matumizi ya al-Qiyaas yalienea kwenye kesi ambapo hamna andiko linalofanana ndani ya Qur-aan au Sunnah na hakuna Swahaabah aliyekataa hili.

b.      Al-Ijma’ pia ilikuwa ikitumika kwa mapana kama ni msingi wa hukumu. Hii ilishajiishwa na ukweli kwamba Maswahaba walikuwa ni wachache, na ilikuwa kwao ni rahisi kukubaliana baina yao. Walitumia al-Ijma’ kwenye kesi nyingi. Kwa mfano; makubaliano yao kwamba Khaliyfah au Imaam ateuliwe, kwamba wanaoritadi wapigwe vita na wauawe, kwamba anayeritadi hawezi kuchukuliwa kama ni mahabusu wa vita, na kwamba hiyo Qur-aan ikusanywe na kuandikwa kuwa ni Kitabu kimoja.

 

 

Share