Uswuul al-Fiqhi al-Islaamiy
Twaaha Jaabir al-‘Alwaaniy
Imetafsiriwa na ’Abdun-Naaswir Hikmany
UTANGULIZI KUTOKA ALHIDAAYA.
Bismillaah waswalaatu was-salaamu 'alaa RasuuliLlaah, wa aalihi wa-aswhaabihi wa ba'ad,
Tumeona umuhimu mkubwa wa kukitafsiri kitabu hichi kutoka somo la Uswuul al-Fiqhi kwani wasomi wengi, Mashaykh na wanafunzi wa Dini wamekuwa hawanufaiki vilivyo na kitabu hichi kwa kukosekana elimu hii kwa lugha ya kiswahili. Hivyo, tunatarajia kwamba kitabu hichi InshaAllaah kiwe na manufaa makubwa haswa kwa wenye uchu wa kutafuta elimu pamoja na Mashaykh kwani ni somo muhimu linalosakwa sana na watafutaji elimu.
Hali kadhalika maelezo yaliyomo ndani ya kitabu hichi ni mepesi kuyasoma na kuyaelewa kwani yapo kwa utangulizi na kitabu hichi hakijaenda ndani sana kuhusiana na somo hilo la Uswuul.
Ni materejeo yetu kwamba kutokana na tafsiri hii, itapatikana faraja kwa wasomi pamoja na kupatikana usomaji uliotanuka kwa wanafunzi wa Uswuul.
Na bila shaka hiki ndicho kitabu cha kwanza cha somo la Uswuul al-Fiqhi kufasiriwa kwa lugha ya kiswahili. Tunaamini InshaAllaah Waislam wengi watanufaika kwa kazi hii na yaliyomo ndani yake.
Mwenyeezi Mungu Amlipe malipo mema Dkt. Twaaha Jaabir al-‘Alwaaniy mwandishi wa kitabu, na kadhalika ndugu yetu mfasiri wa kitabu hiki kwa Kiswahili, al-Akh ’Abdun-Naaswir Hikmany. Tusiwasahau hao wote kwa du'aa InshaAllaah pamoja na wahusika wa AL HIDAAYA ambao wameisimamia kazi hii.
AL-HIDAAYA
»
- Login or register to post comments
- Email this page


