Pilau Ya Nyama Ya Mbuzi Kwa Kachumbari Ya Asili

Pilau Ya Nyama Ya Mbuzi Kwa Kachumbari Ya Asili

 

 

Vipimo:

 

Mchele wa basmati - 3 vikombe

Nyama mbuzi – kilo  2

Viazi - 3

Vitunguu – 5 kata slices

Kitunguu saumu (thomu/garlic) iliyosagwa - 2 vijiko vya supu

Bizari ya pilau nzima (cumin seeds) – Vijiko 3 vya supu 

Mdalasini – kijiti kimoja

Pilipili manga – chembe kiasi

Karafuu nzima – kiasi chembe 7

Hiliki nzima – kiasi chembe 7

Chumvi - kiasi

Mafuta ya kupikia - ¼ kikombe

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:

  1. Osha mchele na roweka  
  2. Changanya nyama na chumvi na tangawizi, kisha chemsha nyama kwa maji kiasi vikombe 6.  Ikiwiva weka kando, na itabakia supu yake kiasi.
  3. Weka mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vikaribie kugeuka rangi.
  4. Tia vipande vya viazi ukaange kidogo.
  5. Tia bizari nzima, pilipili manga, karafuu, kijiti cha mdalasini.
  6. Vuruga hiliki kisha tia pamoja na thomu, uendelee kukaanga kidogo tu.
  7. Mimina mchele kaanga kidogo, kisha mimina nyama na supu yake, maji yawe kiasi ya vikombe 5.
  8. Koroga kisha funika upike pilau kwa moto mdogo wa kiasi hadi iwive.
  9. Pakua utolee kwa kachumbari ya asili.

 

 

Bonyeza Upate Pishi La Kachumbari Ya Asili:

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)

 

Share