Fidia Asiyeweza Kufunga Anaweza Kulipa Baada Ya Ramadhwaan?

 

Fidia Asiyeweza Kufunga Anaweza Kulipa Baada Ya Ramadhwaan?

 

  www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalam aleykum,

Swali langu linahusu FIDIA kwa mtu ambaye hawezi kufunga swaumu ya Ramadhan kwa sababu ya ugonjwa ambao hatarajii kupona ( Kisukari ) na ameshauriwa na daktari aendelee kutumia dawa na asikae bila kula kwa muda mrefu.  

 

SWALI: Endepo Fidia ilicheleweshwa kwa sababu ya hali ya kipato na mwezi wa Ramadhan umekwisha, je anaweza kulipiwa Fidia hata mwezi unaofuata? 

 

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.  

 

Asiyeweza kufunga Ramadhwaan kwa sababu ya ugonjwa unaoendelea au mzee asiyeweza kufunga n.k. ana khiari kutoa fidia katika mwezi wa Ramadhwaan au mwisho wa Ramadhwaan kama alivyoeleza ‘Allaamah Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah). Na anaweza kufanya ifuatavyo:

 

1. Anaweza kulipa kila siku moja kwa kulisha masikini mmoja.

 

 

2. Anaweza kulisha masikini 30 au 29 kwa pamoja kulingana na siku za deni lake. Alifanya hivyo Anas Bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) alipofikia umri mkubwa na akashindwa Swawm alikusanya masikini 30 pamoja na kuwalisha.

 

 

3. Anaweza kulisha maskini huyo huyo mmoja kila siku hadi zitimie siku za deni lake.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share