Mjomba Ameacha Mke, Mjukuu Na ndugu Wa Kike Na Wa Kiume, Wanawe Walifariki Kabla Yake

 SWALI:

Asalam Alaykum!

Shukran kwa website hii yenye manufaa mengi kwa ummah wa Kiislamu. Mwenyezi Mungu awabariki na awape mafanikio nyote.

Nina swali moja, in shaAllaah mutanisaidia. Marhum mjomba wangu alipoaga dunia, aliwacha nyuma warithi mkewe, mjukuu wake wa kike, ndugu wa kiume wawili na ndugu wa kike mmoja. Marhum alikuwa na watoto wa kiume wawili, wote wamefariki kabla yake. Mmoja alifariki kabla hajaona na wapili alipofariki ndio aliacha huyo mjukuu wa kike sasa ana miaka 16.

Marhum amecha mali alipofariki. Je kidini nielezee Mali yake itagawanya vipi? Shukran.

 

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa ndugu yetu muulizaji swali. kwa maelezo uliyotupatia mirathi ya warithi itakuwa kama katika jadwali iliopo chini:

 

 Warithi

Uhusiano na aliyekufa

Kiwango

Hukumu

1

Mke

Thumuni (1/8)

Kwa sababu ya kuweko kwa warithi, yaani watoto anapata kiwango hicho.

2

Kaka 1

3/20

Huyu anazuiliwa kwa kuwepo mjukuu, hivyo baki ya wirathi unagawiwa ndugu wa aliyefariki – mafungu 2 kwa kaka na moja kwa dada.

3

Kaka 2

3/20

 

4

Dada 1

3/40

 

5

Mjukuu wa kike

Nusu (1/2)

Huyu anachukuliwa kama binti, hivyo kupata fungu hilo.

 

 

Huu ndio mgao wa waliobaki katika warithi wa aliyefariki.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share