Akitoka Dar Kwenda Arusha Anaruhusiwa Asifunge
SWALI
Mtu anaesafiri kutoka sehemu moja kwenda nyengine. Naomba ufafanuzi kidogo hapo kuhusu safari. Kilichokusudiwa katika safari ni nini hasa, maana mfano, mi natoka Dsm kwenda Arusha (Kilomita 850) nikitumia gari masaa 8-9 na nikitumia ndege ni saa 1-1.5 tu. naruhuswa kula kwa sababu nasafiri ama hii ni safari ipi hasa ambayo mwenye kufunga anaruhusiwa kula.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu kwa swali lako la tatu. Hakika ni kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Ametuelezea kiujumla kuhusu mtu kutofunga kwa ajili ya safari wala Hakutuekea masafa yoyote na njia ya isafiri. Anasema Aliyetukuka: “Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine” (2: 184).
Kila mmoja wetu anajua safari pindi anapoazimia kufanya hivyo. Hakika ni kuwa wapo watu wanapata shida kwa kusafiri kwa ndege mbali na kuwa muda unakuwa mdogo. Hivyo, ikiwa unakwenda Arusha kutoka
Lakini kutokufunga ni kutumia ruhusa na kufuata Sunnah hivyo itakuwa ni kupata thawabu zaidi kwani usimulizi wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ufuatao unasema:
عن جابر بن عبدالله أن رسول الله صلى الله عليه وسلم رأى رجلا يظلل عليه والزحام عليه فقال : ((لَيْسَ مِنَ الْبِرِّ الصِّيَامُ فِي السَّفرَ)) صحيح أبي داود
Kutoka kwa Jaabir bin 'Abdillaah ambaye amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimuona mtu akiwa amewekwa chini ya kivuli hali yake taabani baada ya kudhoofika kutokana na Swawm akamwambia: ((Sio katika wema (ucha Mungu) kufunga katika safari)) [Swahiyh Abiy Daawuud]
Kwa mwenye kufungua itambidi alipe siku alizokula akiwa katika safari.
Hata ukielekea Morogoro kutoka Dar pia ni safari na sheria imekupatia ruhusa ya kula.
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


