Skip navigation.
Home kabah

Siku Za Kiislamu Zinaazia Saa Ngapi?

 

SWALI:

siku kwa waislam inaanza na kwisha saa ngapi?

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Swali lako la kwanza ni kwamba siku za Kiislamu zinaanza kuhesabika jua linapozama yaani wakati wa Magharibi hivyo kama mfano leo ni siku ya Alkhamiys na Magharibi inapoingia, basi usiku huo huitwa tena Laylatul-Jumu'ah (Usiku wa Ijumaa) na hali kadhalika kwa masiku mengine.

Na si saa sita ya usiku kama ilivyo hali ya siku au tarehe za ki-Gregorian ambayo ni marekebisho ya tarehe zilizokuwa zikijulikana zamani kama tarehe za ki-Julian ambazo ndizo zinazotumika katika ulimwengu leo hii. Nazo hujulikana zaidi kwa wengi kama tarehe za kikristo au tarehe za kizungu! Kubadilika huko kwa siku za Kiislam wakati wa Magharibi, ni kwa sababu tarehe za Kiislam hufuata mwezi na hazifuati jua kama ilivyo hali ya tarehe nyinginezo.

Na Allaah Anajua zaidi