Nini Tofauti Ya Mitihani Ya Binaadamu Na Mitihani Ya Allaah?
|
Mitihani ya Binaadamu |
Mitihani ya Allah
|
|
Inahitajika kusoma vitabu vingi na mwanafunzi inambidi afanye juhudi kubwa na mashaka kusoma hadi apasi mitihani yake
|
Kitabu kimoja tu chepesi kukisoma nacho ni Qur-aan |
|
Mitihani ya binaadamu haijulikani ni maswali yepi yatakayokuja kabla ya mitihani |
Maswali tayari yameshajulikana kama; Nani Mola Wako Ipi Dini Yako Nani Mtume wako? Umeutumiaje ujana wako? Umeipata vipi mali yako na umeitumiaje? Umri wako umeutumia vipi? Elimu yako umeitumiaje?
|
|
Hupewi majibu kabla ya mitihani |
Unapewa majibu tayari hapo hapo unaweza kujua vipi kuyapata na kuyafanyia kazi.
|
|
Waalimu waliochaguliwa kufundisha masomo ya mitihani hiyo wanaweza kukosea
|
Waalimu waliochaguliwa na Allaah kusimamia na kufundisha mitihani, ni Ma’aswumiyn (Wamelindwa na makosa) [nao ni Mitume] |
|
Muda wa mitihani haizidi masaa |
Muda wa mitihani unaweza kufika hadi miaka 70 au zaidi ambao ni umri wa mwana Aadam!
|
|
Fursa ya kurudia mtihani baada ya kufeli ni mara chache tu, hata hivyo hakuna dhamana kuwa ndio kufuzu |
Fursa ya kurudia mtihani ipo wazi hadi kabla ya mauti ya bin Aadam na dhamana ya kufuzu ipo madamu tu utajaribu!
|
|
Daraja unayopewa haizidi 100% |
Daraja yake kubwa ni 700 na Allaah Huzidisha zaidi Atakavyo
|
|
Matokeo yake yaani kufuzu kwake ni ya kidunia pekee |
Matokeo/kufuzu kwake ni duniani na Akhera pia.
|
|
Husahau mtihani baada ya muda |
Hausahauliki kwani umehifadhika katika Lawhum Mahfuudh (ubao uliohifadhiwa)
|
|
Zawadi yake ni karatasi na wino (shahada) ambayo itatoweka tu
|
Zawadi yake ni Pepo ya kudumu daima bila ya kubadilika hali yake |
|
Inabidi utoke uende masafa shuleni au chuoni
|
Unaweza kufanya mtihani ukiwa nyumbani kwako kwa kufanya ibada na kuomba ufuzu |
|
Wakati au tarehe yake ni fulani tu
|
Wakati wowote, siku yoyote katika uhai wako |
|
Masikini anaweza asijimudu kulipia mtihani
|
Masikini au fakiri wote wanaweza kutekeleza mtihani wa Allah |
|
Kunaweza kutokea upendeleo akadhulumiwa bina Aadam asipewe natija anayostahiki
|
Hadhulumiwi mtu hata chembe ya khardal, atalipwa bin Aadam kila kitu! |
|
Kwa hiyo ni maajabu makubwa kwa mtu kufuzu mitihani ya Binaadamu na kufeli mitihani ya Mola Mtukufu! |
|
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
