Mke Aliyesilimu Hataki Kufuata Mafunzo Ya Dini Mara Nyingine Anasema Yeye Sio Muislamu

 

SWALI  

 

 

My question is I have married a converted girl, living together for 4 years now, I  was trying to teach her our religion and before she was listened and followed me like Fasting but Praying was difficult for her, unfortunately now she forgets everything and when-ever I try to teach her she sometimes say she is Christian and not Muslim, we have already one child so Because all of us we are keeper as Qur-an says, I`m afraid to be questioned yaumul qiyyamat, so MY mind says to find another wife, is it a good Idea to do so or since we have a kid EVEN THOUGH she doesn’t listen to me, I have to continue live with her even though she doesn't want to follow the religion? And if so what about the aya which says (and do not marry mushrikina until they believe) THANKS WABILLAHI TAUFIQ.

 

Thanks (jazaka aalah kheir)

 


 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako hilo kuhusu ndoa. Mara nyingi huwa tunawashauri ndugu zetu msiwe ni wenye kufanya haraka ya kuoa asiye Muislamu hata kama ni Ahlul Kitaab tuliokubaliwa kuwaoa kwa sababu zinazoonekana kivitendo katika jamii kwa wale ambao tayari waliokwishawaoa. Pia tunatahadharisha kaka zetu kumuoa binti aliyesilimu na hapo hapo mkafunga Nikaah huku akikuahidi kuwa atakuwa Muislamu mzuri. Jambo ambalo tunataka ndugu zetu wafanye ni baada ya kumsilimisha msichana anatakiwa ampeleke sehemu ya kusoma Dini na hapo awe atakuwa ni mwenye kusoma kwa muda usiopungua miezi sita kisha ndio afunge ndoa baada ya kukinaika na Uislamu wake.

 

Tufahamu kuwa kila Muislamu ni mchunga na kila mchunga ataulizwa alichokichunga, amekielekeza pema au amekipoteza. Nyumba yenye kheri ni ile ambayo baba na mama wanafanya matendo ya Uislamu ili watoto nao waige. Mtoto mliyenaye atainukia na Dini gani au Ijumaa atakwenda Msikitini na Jumapili Kanisani? Tunafahamu kuwa nchi nyingi kunapotokea ugomvi baina ya wanandoa basi mtoto anapatiwa mke. Ikiwa itakuwa hivyo utakwenda kumjibu nini Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala). Jua kuwa lau mtaachana mtoto huenda akapatiwa mama na hivyo kuwa katika matatizo ya kukulia katika Ukristo.

 

Jambo ambalo utafaa uliangalie kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ni kutazama sheria na kanuni za nchi unaoishi. Ikiwa utatoa talaka mtoto atapatiwa nani? Na je, ukizungumza naye kwa utaratibu ukamueleza mazuri ya Uislamu anaweza kubadilika? Je, kubadilika kwake huko tatizo ni wewe kwa kuwa ulikuwa humtimizii mahitaji yake kiukamilifu au ni vipi? Je, ulikuwa ukiishi naye Kiislamu? Jaribu kuyajibu maswali haya na baada ya hapo umpatie muda wa kujirekebisha. Ikiwa atabakia vile vile basi ni bora umuache na utafute Muislamu aliye mcha Mungu.

 

Tunakutakia kila kheri na fanaka katika suala hilo.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share