20-Hadiyth Al-Qudsiy: Malipo Ya Niyyah Ya Kufanya Hasanaat Na Maovu

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 20 

Malipo Ya Niyyah Ya Kufanya Hasanaat Na Maovuu

 

عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيمَا يَرْوِي عَنْ رَبِّهِ عَزَّ وَجَلَّ قَال: ((إِنَّ اللَّهَ كَتَبَ الْحَسَنَاتِ وَالسَّيِّئَاتِ ثُمَّ بَيَّنَ ذَلِكَ، فَمَنْ هَمَّ بِحَسَنَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللَّهُ لَهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً،  فَإِنْ هُوَ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا كَتَبَهَا اللَّهُ لَهُ عِنْدَهُ عَشْرَ حَسَنَاتٍ إِلَى سَبْعِ مِائَةِ ضِعْفٍ، إِلَى أَضْعَافٍ كَثِيرَةٍ،  وَمَنْ هَمَّ بِسَيِّئَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا كَتَبَهَا اللَّهُ لَهُ عِنْدَهُ حَسَنَةً كَامِلَةً، فَإِنْ هُوَ هَمَّ بِهَا فَعَمِلَهَا، كَتَبَهَا اللَّهُ لَهُ سَيِّئَةً وَاحِدَةً)) البخاري و مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kutokana na yale aliyoyapokea kwa Rabb wake Tabaaraka Wa Ta’aalaa kwamba amesema: “Hakika Allaah Ameandika hasanaat (mazuri) na maovu kisha Akayabainisha. Basi atakayetilia hima kufanya hasanah (zuri) moja, kisha asiweze kuifanya, basi Allaah Atamwandikia (thawabu za) hasanah moja kamilifu.  Na ikiwa ametilia hima kuifanya kisha akaifanya, basi Allaah Atamwandikia hasanaat kumi hadi mara mia saba maradufu zaidi ya hayo. Na akitilia hima kufanya ovu moja kisha asifanye, basi Allaah Atamuandikia hasanah moja kamilifu. Na ikiwa akitilia hima akalifanya, basi Allaah Atamuandikia ovu moja.” [Al-Bukhaariy na Muslim kwa herufi hizi]

 

 

 

Share