Hadiyth Ya 42 - Waja Peponi Watapata Ridhaa Ya Allaah
Hadiyth Ya 42
Waja Peponi Watapata Ridhaa Ya Allaah
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ اللَّهَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى يَقُولُ لِأَهْلِ الْجَنَّةِ: يَا أَهْلَ الْجَنَّةِ. فَيَقُولُونَ لَبَّيْكَ رَبَّنَا وَسَعْدَيْكَ. فَيَقُولُ هَلْ رَضِيتُمْ؟ فَيَقُولُونَ وَمَا لَنَا لَا نَرْضَى وَقَدْ أَعْطَيْتَنَا مَا لَمْ تُعْطِ أَحَدًا مِنْ خَلْقِكَز فَيَقُولُ: أَنَا أُعْطِيكُمْ أَفْضَلَ مِنْ ذَلِكَ. قَالُوا: يَا رَبِّ وَأَيُّ شَيْءٍ أَفْضَلُ مِنْ ذَلِكَ؟ فَيَقُولُ: أُحِلُّ عَلَيْكُمْ رِضْوَانِي فَلَا أَسْخَطُ عَلَيْكُمْ بَعْدَهُ أَبَدًا)) البخاري, مسلم و الترمذي
Kutoka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudriyyرضي الله عنه ambaye kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: ((Allaah تَبَارَكَ وَتَعَالَى Atawaambia watu wa peponi: Enyi watu wa Peponi! Watasema: Labeka Mola wetu tuko kwa ajili ya amri Yako. Kheri yote imo katika mikono Yako. Kisha Atasema: Je, mmeridhika? Watasema: Vipi tusiridhike na hali Umetupa ambayo Hukumpa yeyote mwengine katika viumbe Vyako? Kisha Atasema: Nitakupeni kilicho bora kuliko hayo. Watasema: Ee Mola, ni kipi kilicho bora kuliko haya? Atasema: Nitafanya ridhaa (mapenzi) Yangu iwateremkie na baada ya hapo Sitokasirika nanyi tena
- Login or register to post comments
- Email this page


