Chapati -2

Chapati -2

     

Vipimo   

Unga wa ngano mweupe - 1 Kilo

 

Samli - 150gm

 

Chumvi - 3 vya chai

 

Maji ya moto yasichemke lakini -  Kiasi

 

Mafuta Ya Zaituni (olive oil)- 4 vijiko vya supu

 

Samli tena - 200 gms

 

Iliki iliyosagwa - 1 kijiko cha chai

  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika     

  1. Tia unga  kwenye sinia au bakuli kubwa lilo na nafasi, changanya na chumvi, mafuta ya zaituni, samli 150g, iliki, mimina maji ya moto kwa kipimo cha kikombe kila unapovuruga unga. 
  2. Uunga uwe  mwepesi unapoganda kuwa donge moja kubwa. Uwache kwa muda wa dakika 60 (saa moja hivi) ukiwa umeufinika ili unga ulainike.  
  3. Katakata madonge makubwa yenye ukubwa wa chungwa  ili uweze kutoa kila donge chapati mbili. Ukimaliza hapa weka madonge kwa muda wa nusu saa ukiwa umefinika bila ya kuingia upepo ndani.
  4. Sukuma donge ukiwa umelimwagia unga mkavu juu, liwe mviringo. Unaweza kutumia kifimbo   hata chupa  kusukumia madonge ikiwa huna kifimbo juu ya meza au kwenye kibao maalumu cha chapati. 
  5. Yayusha samli nyingine ya 200gm  kisha itumie kwa kupaka kwenye kila donge ukilisukuma duara itakayobakia weka kando utachomea chapatti.
  6. Likate katikati kwa kidole chako au kijiko upate mgawanyo wa sehemu mbili sasa kila sehemu utakunja kwanzia ncha moja hadi ikutane na ncha nyengine kama mkeka, donge lake linakuwa na sampuli, huuitwa tabaki mkunjo huu kama ilivyo katika picha. 

     

  1. Weka chuma cha kuchomea chapati jikoni moto mdogomdogo. 
  2. Sukuma kila donge  kisha mara nyengine mviringo huu utakuwa mviringo wa kuchoma weka chapati kwenye chuma kavu bila samli  iache muda wa dakika tatu igeuze upande mwengine kisha vilevile ,  ukiona ina mabapa ya kuchomeka tia samli ile uloyeyusha kwa kijiko kikubwa kimoja huku unaizungusha zungusha.   
  3. Geuza upande wa pili vile vile mpaka iwive. 
  4. Zipange kwenye sahani huku unazifinika, hapa tayari kuliwa kwa mchuzi au mboga yoyote. 

Kidokezo: 

Ukipenda kuzichambua kidogo chapati baada ya kumaliza hii unazishika zote kwa pamoja ikiwa umezikunja, unakunja ngumi au kifimbo kupiga tu mara moja tosha.

 

 

Share