Vipi Kuwakinga Watoto Na Mashaytwaan?SWALI:

vipi alikua mtume s.a.w akiwakinga wajuku zake na sheitwani?

 


 

JIBU:

Sifa zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad  صلى الله عليه وآله وسلمna Swahaba zake  رضي الله عنهم  na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

Du'aa inayo kingwa nayo watoto.

Imepokelewa  na Ibn Abbas amesema  alikuwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akiwakinga wajukuu wake (Al-Hasan na Al-Husayn) akisema :

 

أُعيـذُكُمـا بِكَلِـماتِ اللهِ التّـامَّة، مِنْ كُلِّ شَيْـطانٍ وَهـامَّة، وَمِنْ كُـلِّ عَـيْنٍ لامَّـة


 

U'iydhukuma Bikalimati-Llahit-Taammati min kulli shaytwaanin wa haammah, wa min kulli 'aynin laamah.
 

“Nawakinga kwa maneno ya  Allah  yaliyotimia Awakinge kutokana na kila shaytwaan na uvamizi na kila jicho lenye kudhuru”

 

Na Allah Anajua zaidi.

 

Share