Biskuti Nyembamba (Wafer Bar) Za Chokoleti Na Njugu

Biskuti Nyembamba (Wafer Bar) Za Chokoleti Na Njugu

 

  

Vipimo  

Wafer Powder/gram wafer  (unga wa biskuti uliosagwa wa tayari) - vikombe 2

Maziwa ya Mgando Matamu ya Kopo - 2 vikombe

Nazi iliyokunwa  - ½ Kikombe  

Chokoleti  vipande vipande -  1 Kikombe  

Njugu vipande vipande -   ½ Kikombe

Siagi - 227 g

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Yeyusha siagi motoni kisha changanya na unga wa wafer acha kidogo motoni
  2. Mimina katika treya unayochomea itandaze vizuri, kisha mimina maziwa juu yake pamoja na njugu vipande , nazi iliyokunwa na vipande vya chokoleti.
  3. Choma (bake) kwenye oveni kwa moto wa 350ºC kwa dakika 20.
  4. Katakata tayari kwa kuliwa

 

 

 

Share