Vibiskuti Vya Siagi
VIPIMO
Unga 2 Vikombe
Sukari ya icing 1 Kikombe
Siagi 250 gm
Yai 1
Vanilla 2 Vijiko vya chai
Baking powder 1 Kijiko cha chai
Jam ¼ kikombe
Lozi ¼ kikombe
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).
2. Tia yai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini kama sufi.
3. Tia unga na baking powder changanya na mwiko.
4. Chota mchanganyiko kwa mkono (kiasi cha kijiko kimoja cha supufanya duara kisha weka kwenye treya ya kupikia.
5. Bonyeza kila kiduara katikati kwa kidole, kisha weka jam na tupia lozi zilizomenywa na kukatwa katwa.
6. Pika (bake) katika oven moto wa 375° F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.
»
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha



mimi ni mwanachama wa
mimi ni mwanachama wa alhidaaya kutoka kenya lakini wakati huu niko sweden ,je naweza kupata kijitabu kilicho na pamishi haya mazuri ninayo yaona ilinitumie jikoni kutayarisha vyakula mbalimbali
Tumepokea ombi lako lakini
Tumepokea ombi lako lakini tunasikitika kuwa hapa sipo mahali pa kutuma maombi bali ni sehemu ya kuweka maoni kuhusiana na Makala mbali mbali n.k. Mfano hapa ilipasa uweke maoni kuhusu huu upishi wa biskuti.
Mnatakiwa muwe mnaingia sehemu ya 'Wasiliana Na Sisi ' iliyoko hapo juu kisha utume maombi au maswali kwa kutumia anuani inayohusika kama 'Tuma Mapishi' n.k.
Ama kuhusu kitabu cha mapishi, tunapenda kuwajulisha kwamba haya mapishi hayamo katika kitabu chochote, bali ni mapishi yanayoandaliwa nyumbani na kupigwa picha na kuyaweka. Na lau kama tungelikuwa na uwezo tungeliyatengenezea kitabu chake lakini ni jambo linalohitaji gharama na muda mwingi.
Ndugu Zenu
AL HIDAAYA