Anaweza Kumuingilia Mkewe Katika Muda Anaonyonyesha Au Haifai?

SWALI:

 

Assalaam Aleykum Mimi ni kijana wa kiislam nimeoa nina mtoto mmoja .Swalilangu ni je inafaa kumwingilia mke wangu wakati ana mtoto wa miezi mwili na  kama haifai ni inafaa baada ya muda gani? 2 Je ni kweli kwamba kufanya

jimai wakati mke ananyonyesha kunamuathiri mtoto? WABILAH TAWFIQ   

 

 


 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Tumepokea Swali lako, na ingawa zamu yako haikufika bado ya kujibiwa kwa sababu kuna maswali mengi nyuma yako yaliyoingia, tunakujibu haraka  kutokana na umuhimu wa Swali wa kujizuia haki yako kwa jambo ambalo sio kweli.  

 

Umefanya vizuri kuuliza jambo kama hili ambalo halina dalili, bali ni kauli tu za watu wanaojisemea bila ya elimu na kuwasababisha watu kukosa kutimiza haki zao.

 

Hakuna makatazo ya kutokumuingia mke akiwa na mtoto mchanga au akiwa katika muda wa kunyonyesha. Unaweza  kumuingilia mkeo wakati wowote ule pale tu akisita damu yake ya nifaas. Inampasa afanye ghuslu (kuoga josho) kwa maana ajitie twahara hata ikiwa ni siku chache baada ya kujifungua madamu damu imesita basi ameshakuwa ni mwenye kupasi kuswali, kufunga na mumewe anaweza kumuingilia wakati wowote apendao.

 

 

Ingia katika viungo vifutavyo upate maelezo zaidi kuhusu mas-ala haya.

 

Yanayohusu Hedhi Na Nifaas

 

 Muda Wa Kutwaharika Na Damu Ya Nifasi

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share