Nini Tofauti Ya Nabii (An-Nabiyy) Na Mjumbe (Ar-Rasuul)?

SWALI:

 

ASALAM ALAIKUM WARAHMATULLAHI TAALA WABARAKATU ALAH AKULIPENI KWA KUTUSAIDIA ELIMU HII KWA NJIA YA ALHIDAAYA AWAPE WEPESI NA KUWAWEZESHA MPATE NA CHANNEL ITAYORUSHWA HEWANI INSHAALAH SWALI LANGU: NINI TOFAUTI YA NABII NA MJUMBE AU MTUME


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu tofauti baina ya Nabii na Rasuul (Mjumbe). Wanachuoni wetu wamezungumza mengi kuhusu tofauti baina ya maneno hayo mawili. Hata hivyo, tofauti ya maneno kwa usahali na wepesi ni kuwa Nabii ni mjumbe aliyetumwa na Allaah Aliyetukuka bila kuteremshiwa sheria au kanuni mpya ilhali Rasuul ni yule aliyeteremshiwa sheria mpya. Hivyo, Nabii hutumia sheria ya Mtume aliyemtangulia.

 

Kwa ufupi ni kuwa kila Mtume ni Nabii lakini si kila Nabii ni Mtume. Mtume ana daraja kubwa kuliko Nabii.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share