Dua Ya Kutawadha
SWALI:
Ukitia wudhuu na ukasahau kusoma dua inayotakiwa katika kiungo fulani, je, unaweza kurudia kiungo hicho mathan ikiwa hujafika mbali?
JIBU
Hakuna dua ya kutawadha kila kiungo katika wudhuu, akifanya mtu hivyo basi atakuwa amefanya bid'aa kwani hayo ya kusoma Dua yamekuja katika mapokezi dhaifu yasiyotegemeleka. Dua ni mwanzo tu unasema Bismillah ambayo ni lazima
((عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال لا وضوء لمن لم يذكر اسم الله تعالى)) رواه أبو داود.
((Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه kwamba amesema Mtume صلى الله عليه وسلم : Hakuna wudhuu kwa asiyetaja jina la Allaah سبحانه وتعالى )) Abu Dawuud
Ukishaanza wudhuu basi hakuna tena dua yeyote ila baada ya kumaliza wudhuu ambapo unasoma dua yake ya kupata fadhila za kufunguliwa milango minane ya pepo
((عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ما منكم من أحد يتوضأ فيسبغ الوضوء ثم يقول أشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له وأشهد أن محمداً عبده ورسوله اللهم اجعلني من التوابين واجعلني من المتطهرين إلا فتحت له أبواب الجنة الثمانية يدخل من أيها شاء )) رواه الترمذي
((Imetoka kwa 'Umar رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وسلم kasema: Hakuna katika mmoja wenu atakayetawadha akautengeneza wudhuu kikamilifu, kisha akasema :
(Ash-hadu alla Ilaaha illa Allaah wahdahu laa shariyka
“Nakiri kwa moyo na kwa kauli kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu peke yake, wala Hana mshirika wake, na ninakiri kwamba Muhammad صلى الله عليه وسلم ni mja wake na ni Mtume wake” “Ewe Mwenyezi Mungu nijaalie niwe miongoni mwa wale wanaoomba msamaha, na nijaalie miongoni mwa wale waliosafi" isipokuwa atafunguliwa milango minane ya pepo aingie wowote autakao )) At-Tirmidhiy
Na hizi ni adabu na dua za kuingia chooni na kutoka pamoja na wudhuu
Dua ya kuingia chooni
(Ingia kwa kutanguliza mguu wa kushoto)
(بِسْمِ الله ) اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِـكَ مِـنَ الْخُـبْثِ وَالْخَبائِث
“(Kwa jina la Mwenyezi Mungu ) Ewe Mwenyezi Mungu najilinda kwako kutokana na mashetani ya kiume na ya kike”
Dua ya kutoka chooni
(Unapotoka anza kutanguliza mguu wa kulia)
غُفْـرانَك
“Nakuomba msamaha (Ewe Mwenyezi Mungu)
Dua ya kabla kutawadha
بِسْمِ الله
“Kwa jina la Mwenyezi Mungu (nina tawadha)
Dua baada ya kutawadha
أَشْهَدُ أَنْ لا إِلَـهَ إِلاّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَريـكَ لَـهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمّـداً عَبْـدُهُ وَرَسـولُـهُ
“Nakiri kwa moyo na kwa kauli kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu peke yake, wala Hana mshirika wake, na ninakiri kwamba Muhammad صلى الله عليه وسلم ni mja wake na ni Mtume wake”
اللّهُـمَّ اجْعَلنـِي مِنَ التَّـوّابينَ وَاجْعَـلْني مِنَ المتَطَهّـرِينَ
“Ewe Mwenyezi Mungu nijaalie niwe miongoni mwa wale wanaoomba msamaha, na nijaalie ni miongoni mwa wale walio
سُبْحـانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْك
“Utakatifu ni Wako, Ewe Mola wangu, na shukurani zote zinarudi Kwako, nakiri kwamba hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Wewe, naomba msamaha wako, na narejea kwako (kwa kutubia )”
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


