Inafaa Kuswali Sunnah Kabla Ya Swalah Ya Magharibi?

SWALI

 

a'allykum warahmatullah wabarakatuh

 

mimi swali langu ni hili hapa nina mama yangu anaomba jibu lenu anasema huwa anasali sala ya sunna kabla maghrib nabaada ya maghrib na kaambiwa haifai lakini bado anaendlea sasa je ni makosa au aendelee tu mana yuko katika njia panda hajui afanye nini?wabillah taufiq inshaallah allah atakupeni wepesi wa kujibu maswali yetu yote ameen
 

 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Hakuna makatazo ya kuswali Sunnah kabla ya Magharibi au baada ya Maghrib bali inapendekezeka kufanya hivyo. Ila huenda imefahamika kwa aliyemkataza kuswali, kuwa ni kabla ya kuadhiniwa Magharibi, kwa maana baada ya Swalaah ya Alasiri. Ikiwa hivyo basi itakuwa haifai  kwani wakati huo ni miongoni mwa nyakati ambazo  makruuh (zinazochukiza kuswali), hivyo hakuna Swalaah ya Sunnah. Lakini baada ya kuadhiniwa Magharibi inafaa kuswali Sunnah ambayo inajulikana kuwa Sunnah Ghayr Muakkadah (Sunnah isiyosisitizwa).

Tafadhali ingia katika kiungo kifutacho upate ratiba ya Swalah za Sunnah zote ambazo zimetajwa pia hizo Sunnah mbili za kabla ya Magahribi na baada yake.

Ratiba Ya Swalah Za Sunnah Zilizosisitizwa Na Zisizosisitizwa

 Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share