Kuishi Na Mume Aliyeritadi Kwa Ajili Kumhudumia Ugonjwa

SWALI:

 

 

MIMI NI MAMA MWENYE WATOTO WAWILI AMBAYE UMRI WANGU NI MIAKA 35 NIMEOLEWA, MUME WANGU ALIPATA MATATIZO MWAKA 2002 ALIUGUA STROKE SASA BAADA YA HAPO ALIBADILISHA DINI NA KUWA MKIRISTO NA MIMI BADO MWISLAMU NA NAFUNGA SWAUMU KAMA KAWAIDA NA HUYU MUME WANGU NAISHI NAE HADI LEO HII NA BADO ANAUMWA NA HATUJASHIRIKI TENDO LA NDOA YAPATA MIAKA SITA SASA.

 

JE SWAUMU YANGU INASWIHI, PIA NDOA YANGU IKO KATIKA HALI MAANA SIELEWI KWANI SIWEZI KUONDOKA HALI YA MGONJWA SI NZURI JE NIFANYEJE? WASALAMU ALEIKUMU WAALAHMATULLAH WABARAKATU


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuritadi kwa mume wako.

Hakika ni kuwa mume anaporitadi tu ndoa inakatika na hakuna tena ndoa baina yako na yeye. Kwa wakati huo inabidi utoke kwenye nyumba pamoja na watoto ili mtazame mustakbali wenu bila ya mume huyo.

 

Inafaa atazamwe ugonjwa wake na jamaa zake au wahudumu na wala sio wewe. Hiyo ni kuwa kwa sasa huyo si mumeo na kisheria haifai kwako kumhudumikia kwa chochote. Lau atarudi katika Dini basi mnaweza kufunga ndoa tena upya. Inabidi kwa sasa tena utoke katika nyumba hiyo na urudi kwenu.

 

Ama kuhusu Swawm yako na ibada nyinginezo inshaAllaah zinakubaliwa na Allaah Aliyetukuka na hazina matatizo yoyote.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share