Inafaa Kutumia Mali Ya Mume Bila Ya Ruhusa Yake?

SWALI:

 

Inafaa ku tumia mali ya mume nitakavyo? Bila ruhsa yake.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kutumia mali ya mume bila ruhusa yake.

Hakika ni kuwa Haifai kwa mke kutumia mali ya mumewe bila ya ruhusa yake. Inafaa uombe ruhusa katika hilo isipokuwa ikiwa amekupatia ruhusa.

 

Wakati tu ambao unaruhusiwa kutumia ni ule wakati ambao mume ni bakhili na hakupi matumizi na kukutosha wewe na watoto wako. Hilo lilitokea wakati Hind bint ‘Utbah (Radhiya Allaahu ‘anha) alipokwenda kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumshitakia kuwa mumewe, Abu Sufyaan (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa hampi pesa za kumtosha yeye pamoja na watoto. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimpatia ruhusa ya kuchukua kutoka kwa mumewe kwa wema, yaani zinazomtosha na wala asiwe ni mwenye kufanya israfu katika hilo.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share