Zamu Za Wake Wenza

SWALI:

 

Asalam alaykum?

 

mimi ni mwiislamu natatizo langu naomba munisaidia ili nipate kujua. Mume wangu ana wake 2. alipata safari kidoko kwa muda wa siku 2 siku aloondoka ilikuwa kamaliza zamu ya nyumba kubwa na akaa siku 2 hukoalipo kwenda je atakapo rudi ataanza vipi? naomba munifafanulia. naomba nijibiwe kwenye email yangu siyo kwenye website yetu tafadhali.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu zamu za mume baina ya wake.

Ni lazima mtu mwenye wake wawili ni lazima afanye uadilifu wa hali ya juu katika kugawa siku. Ugawaji wa siku ni lazima uwe sawa baina ya wake.

 

Ugawaji huo unaweza kuwa siku moja kwa mke mkubwa na nyengine kwa mke mdogo. Au mtu anaweza kugawa siku mbili mbili au wiki wiki. Katika kesi yako, zamu ya mume baada ya kurudi inaweza kuwa katika hali mbili zifuatazo:

 

1.     Kwako, kwani alipoondoka alikuwa tayari amekaa kwa mke mkubwa siku mbili zake. Kwa hivyo, akirudi ataanza kwako.

2.     Kwa mke mkubwa, kwani siku mbili za safari alikuwa awe kwako na akasafiri na hilo linaweza kumtokea pia mke mkubwa mara nyengine.

 

Njia iliyo muafaka kabisa ni suala hilo mume kujadili na mke mkubwa na kisha na yule mdogo watazame watafuata utaratibu gani ikiwa mume atasafiri, utaratibu wa kwanza au wa pili. Kufanya vikao hivyo kutaondoa utata, na kuweka utulivu baina ya kila mmoja wenu.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share